• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya uagizaji wa huduma wa China katika miaka 5 ijayo yatarajiwa kufikia dola za kimarekani trilioni 2.5

    (GMT+08:00) 2020-11-09 18:54:21

    Wizara ya biashara ya China imetoa ripoti ya mwaka 2020 ya uagizaji huduma kutoka nje ya China. Ripoti hiyo inakadiria kuwa, kutokana na China kuendelea kupanua wigo wa utoaji idhini ya kuingia kwenye soko la huduma na kuongeza uagizaji wa huduma, katika miaka mitano ijayo thamani ya uagizaji wa huduma wa China inatarajiwa kufikia dola za kimarekani trilioni 2.5, ambayo itachukua asilimia zaidi 10 ya thamani ya jumla duniani.

    Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, tangu mwishoni mwa mwaka 2001 China ilipojiunga na Shirika la Biashara Duniani WTO, China imeagiza huduma kutoka nje zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 4.7, ambalo ni ongezeko la wastani la asilimia 15.2 kwa mwaka, kiasi ambacho ni juu kuliko kiwango cha wastani cha dunia, asilimia 7.7. China imekuwa msukumo mkubwa wa kwanza wa kuhimiza ongezeko la uagizaji wa huduma duniani.

    Kwa mujibu wa Benki ya Dunia na mashirika ya Umoja wa Mataifa, mwaka 2019 uagizaji wa huduma wa China umetoa nafasi zaidi milioni 18 za ajira kwa wenzi wake wa biashara, ikiwemo nafasi laki 4 kwa nchi za Afrika, na nafasi milioni 3 kwa nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako