• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFRIKA: OKONJO-IWEALA ANATARIJIWA KUCHAGULIWA KUONGOZA WTO

    (GMT+08:00) 2020-11-09 19:21:50
    Mwanamke na Mwafrika wa kwanza Okonjo-Iweala, anatarajiwa kuchaguliwa kuongoza Shirika la Biashara Duniani (WTO). Mpinzani wa bi Okonjo ni mwanamke mwenzake kutoka korea ya Kusini, Yo Myung-hee.

    Rais Donald Trump wa Marekani alifanya kila mbinu ili kuzuia kuchaguliwa kwa Okonjo-Iweala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WTO, huku akionyesha waziwazi kumuunga mkono Waziri huyo wa Biashara wa Korea ya Kusini.

    Taarifa zinaeleza kuwa, hata hiyo Kamisheni ya Ulaya na Umoja wa Afrika (AU) zimepaza sauti zao na kumuunga mkono Ngozi Okonjo-Iweala ambae ni raia wa Nigeria.

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alisema kuwa, umoja huo unamuunga mkono mgombea huyo raia wa Nigeria na kwamba AU inaamini kuwa WTO haitakwamishwa na lolote katika kupata chaguo sahihi kwa ajili ya kuliongoza shirika hilo.

    Donald Trump mara kwa mara alikuwa akilikosoa Shirika hilo na kuzuia kuteuliwa majaji wapya, hivyo kusababisha kushindwa kuchukuliwa maamuzi kutokana na kukosekana idadi ya majaji inayohitajika.

    Inasemekana kwa kiasi kikubwa kwamba, Joe Biden ambaye ameibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa Rais wa Marekani, atarekebisha haraka uhusiano wa nchi hiyo na taasisi mbalimbali za kimataifa likiwemo shirika la WTO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako