Timu ya wataalamu wa matibabu wa China kimefunga safari kwenda Gambia kuisaidia nchi hiyo kupambana na janga la virusi vya Corona kwa muda wa miezi mitatu.
Timu hiyo ina wataalam 9 wa magonjwa mahututi, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya kupumua, uuguzi, usimamizi wa maambukizi hospitali na kinga dhidi ya maambukizi. Wataalam hao watatoa maelekezo kuhusu kinga na udhibiti wa COVID-19 na pia kushiriki kwenye kazi za matibabu nchini Gambia.
Habari zinasema timu ya nne ya matibabu ya China nchini Gambia itakuwa inafanya kazi za matibabu huko kwa muda wa mwaka mmoja.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |