• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa msukumo zaidi kwa ufufukaji wa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-11-09 20:13:10

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin leo amesema China itashikilia kuhimiza kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, na kuhimiza ufufukaji wa uchumi duniani.

    Takwimu zilizotolewa hivi karibuni kutoka idara ya takwimu ya China, wizara ya biashara na idara kuu ya forodha zinaonyesha kuwa, uchumi wa China unafufuka kwa hatua madhubuti.

    Bw. Wang Wenbin amesema hivi sasa China imepata mafanikio makubwa katika kinga na udhibiti wa virusi vya Corona, shughuli za uchumi na jamii zinaendelea kufufuka kwa hatua madhubuti, hali ambayo inaonyesha uwezo mkubwa wa uchumi wa China. Mashirika ya kimataifa yanakadiria kuwa, China itakuwa nchi pekee yenye uchumi mkubwa duniani inayodumisha ongezeko la uchumi mwaka huu.

    Amesisitiza kuwa baada ya kufufuka kwa uchumi wa China na kuanzishwa kwa muundo mpya wa maendeleo, umuhimu wa China wa kuhimiza ongezeko la uchumi duniani utaonekana zaidi. China itashirikiana na nchi mbalimbali kuimarisha ushirikiano wa kinga na udhibiti wa virusi vya Corona, kulinda utulivu wa mnyororo wa uzalishaji na ugavi duniani, kushikilia kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, ili kutoa msukumo zaidi kwa ufufukaji wa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako