• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kushughulikia kesi za ufisadi

    (GMT+08:00) 2020-11-10 08:47:02

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana aliitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ODPP kuzingatia zaidi kufanikisha mashtaka ya kesi za vigogo hasa zinazohusu matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

    Akiongea mjini Nairobi wakati anapokea ripoti za utendaji kazi za mwaka 2017-2018 na 2018-2019 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji, rais Kenyatta amesema kupitia kufanikisha mashtaka ya kesi hizo ndio ofisi hiyo itaweza kuaminiwa na Wakenya. Pia ameipongeza ofisi hiyo kwa mafanikio iliyopata katika miaka miwili iliyopita baada ya kuanzishwa kwake, na kuihamasisha kushirikiana zaidi na mashirika mengine ya kisheria ili kupata mafanikio makubhwa zaidi katika siku za mbele.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako