• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia haitatumbukia kwenye machafuko kwasababu ya operesheni ya Tigray

    (GMT+08:00) 2020-11-10 08:47:23

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed jana Jumatatu alisisitiza kuwa wasiwasi wa jamii ya kimataifa kwamba Ethiopia inaweza kutumbukia kwenye machafuko kufuatia hatua za kijeshi zinazochukuliwa, hauna msingi na unatokana na kutoelewa lengo lao kwa undani.

    Toka Jumatano iliyopita, serikali ya Ethiopia ilianza operesheni ya kijeshi dhidi ya TPLF, chama tawala katika jimbo la Tigray ambacho kimeanza rasmi mapigano na serikali kuu. Hali hii imezusha hofu ya baadhi ya jamii ya kimataifa kwamba inaweza kuitumbukiza Ethiopia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuleta usumbufu katika pembe ya Afrika.

    Wakati huohuo Umoja wa Mataifa na washirika wake wamesema watabaki kusaidia zaidi ya watu milioni 2 wa eneo lenye mapambano la Tigray wakati ambao mashirika ya kimataifa yanaondoa wafanyakazi wake wasio na umuhimu mkubwa. Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu OCHA imesema mazungumzo yanaendelea kuwaondoa wafanyakazi wake kwenye maeneo yenye mgogoro au yaliyo jirani na hapo na kuweza kuwafikia wale wenye mahitaji, hasa wakimbizi na wale waliokosa makazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako