• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufuata desturi ya kimataifa juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-11-10 09:04:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana alisema kuwa, China itafuata desturi ya kimataifa juu ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani.

    Akijibu swali kwenye mkutano na wanahabari kuhusu lini China itatuma salamu za pongezi Bw. Wang alisema serikali ya China imeona kuwa Bw. Biden ametangazwa kushinda uchaguzi, na inaelewa matokeo ya uchaguzi huo yataamuliwa kwa kufuata sheria na utaratibu za Marekani.

    Aidha amesisitiza kuwa China na Marekani zinapaswa kuimarisha mawasiliano na mazungumzo, kushughulikia tofauti kwenye msingi wa kuheshimiana, kupanua ushirikiano kwa msingi wa kunufaishana, na kukuza uhusiano imara wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako