Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Bw. Mabula Nyanda jana alisema kuwa, watu wasiopungua 50 wanauawa na wanyamapori kila mwaka nchini Tanzania.
Bw. Nyanda alisema wanyama pori waliotoka kwenye eneo la uhifadhi na kupotea pia wanaharibu hekta 5,000 za mazao ya kilimo kila mwaka. Alibainisha kuwa idadi ya watu wanaouawa na wanyamapori inaongezeka na inapaswa kuchukuliwa hatua za haraka ili kushughulikia hali hii ya kutisha. Kamishna huyo amesema TAWA imeshaandaa mpango unaolenga kudhibiti migogoro ya watu na wanyamapori ambayo inaathiri vibaya binadamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |