• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi atuma barua ya pongezi kwenye mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2020-11-10 14:36:27

    Rais wa China Xi Jinping leo ametuma barua ya pongezi kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Jukwaa la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi ISTIF la Baraza la Boao la Asia BFA.

    Akibanisha kwamba dunia inakabiliwa na janga la COVID-19 na changamoto nyingine mbalimbali, rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na nchi nyingine duniani kuimarisha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia pamoja na ushirikiano, na kuongeza mabadilishano ya kimataifa ya uwazi zaidi, shirikishi zaidi na ya kunufaishana kwenye eneo hilo, ili kuchangia katika kuhimiza kufufua uchumi duniani na kulinda afya za watu.

    Rais Xi amesema sayansi na teknolojia vinapaswa kunufaisha watu wote, na kwamba mkutano wa ISTIF unaondaliwa na BFA na mkoa wa utawala maalumu wa Macao utatoa jukwaa muhimu la mabadilishano duniani na ushirikiano kwenye uvumbuzi wa saynsi na teknolonia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako