• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa SCO asema uchumi wa China ni mfano wa kuigwa kwa dunia

    (GMT+08:00) 2020-11-10 19:43:22

    Mkutano wa 20 wa viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai umefanyika leo kwa njia ya video. Shirika kuu la Utangazaji la China CMG limefanya mahojiano na katibu mkuu wa shirika hilo Bw. Vladmimir Imamovich Norov.

    Bw. Norov amesema wakuu wa China, serikali, mashirika ya kijamii na idara za afya wamechukua hatua kwa haraka kulidhibiti janga la virusi vya Corona ndani ya muda mfupi. Jambo ambalo limeonesha uzalendo na ujasiri wa wachina. Mpango wa kugundua, kuripoti, kutenga na kutibu mapema, umehakikisha mafanikio hayo.

    Akiongea kuhusu athari ya uchumi wa China kwa dunia, Bw. Norov amesema janga hilo limeharakisha mchakato wa maendeleo ya uchumi wa kidijitali nchini China. China imejenga mfumo wake wa soko kupitia teknolojia za kisasa na ushirikiano, ambao umetoa mfano wa kuigwa kwa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako