Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Kenya Bw. Macharia Kamau amesema, kuna fursa nyingi kati ya Kenya na Somalia.
Akitolea mfano sekta ya utalii, Bw. Macharia alisema, Kenya inapokea watalii karibu 32,000 kutoka Somalia kila mwaka, lakini sekta ya utalii bado haijapata maendeleo makubwa. Kama sera ya kutoa viza baada ya kuwasili ikitekelezwa, idadi ya watalii kutoka Somalia huenda itaongezeka mara mbili. Aidha alisema kuwa, Somalia hivi sasa inaendelea kubadilisha uchumi wake, na huenda itakuwa mwenzi muhimu wa Kenya katika uchumi, biashara na ushirikiano, na itakuwa chanzo muhimu cha mapato ya utalii na hoteli cha Kenya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |