• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa afya wa Sudan apata COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-11-11 09:33:40

    Kaimu waziri wa Afya wa Sudan Osama Ahmed Abdul Rahim pamoja na mkurugenzi mkuu wa huduma ya msingi ya afya na mkurugenzi mkuu msimamizi wa dawa za kimatibabu wa wizara ya Afya wamepata ugonjwa wa COVIDI-19.

    Ikitoa taarifa wizara ya afya imesema watu hao walioathiriwa wanapatiwa matibabu na wapo kwenye hali nzuri, na kwamba waziri wa afya anaendelea na kazi zake akiwa kwenye kituo cha karantini. Wakati huohuo, kamati ya juu ya dharura za afya nchini Sudan imewataka wananchi kupunguza mikusanyiko na safari katika kipindi cha sikukuu ili kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo.

    Sudan ina watu 707 walioambikizwa COVID-19 tangu mwanzoni mwa Novemba, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na mwanzoni mwa wimbi la kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako