• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhimiza upatikanaji sawa wa chanjo ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-11-11 09:34:01

    Kenya jana ilitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhimiza upatikanaji sawa wa chanjo ya COVID-19 kufuatia matokeo mapya ya majaribio yaliyofanywa na watengenezaji wanaoongoza.

    Patrick Amoth, mkurugenzi mkuu wa afya katika Wizara ya Afya ya Kenya amesema Kenya inakaribisha tangazo hilo la maendeleo ya chanjo yenye ufanisi na iliyo salama, ambayo itaharakisha juhudi za kudhibiti janga. Amesisitiza kuwa chanjo ya COVID-19 ni bidhaa ya afya ya umma duniani ambayo inapaswa kupatikana kwa usawa na nchi. Pia amethibitisha tena uungaji mkono wa Kenya kwa WHO kama shirika maalumu la Umoja wa Matifa linaloratibu afya ya dunia na dharura za afya duniani.

    Amoth amesema Kenya, chini ya usimamizi wa kamati ya mwitikio wa dharura za kitaifa juu ya COVID-19 inatekeleza mikakati ya kina inayolenga kukabiliana na kuenea kwa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako