• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa wa Ethiopia asema operesheni ya kijeshi kaskazini mwa nchi inalenga kuokoa taifa

    (GMT+08:00) 2020-11-11 09:34:19

    Afisa wa Ethiopia amesema operesheni ya kijeshi inayoendelea katika sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo inalenga kuokoa taifa.

    Akiongea na wanahabari, Redwan Hussein ambaye ni msemaji wa Kikosi cha Hali ya Dharura cha Taifa kilichoanzishwa kwa ajili ya Tigray amesema madhumuni ya kuanzishwa kwa operesheni ya kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo wiki iliyopita ni kuiokoa nchi, mamlaka ya nchi na kuhakikisha nchi inashikamana pamoja na baadaye kukaa chini na kuongea na yeyote mwenye ugomvi na serikali.

    Hussein amesema chama cha TPLF kimepora silaha nzito kutoka jeshini, ambapo serikali inalenga kuhakikisha silaha hizo hazitumiki kwa Waethiopia na watu wa nje ya Ethiopia. Amesema serikali imetangaza kukamata roketi na makombora yenye uwezo wa kwenda kilomita 300, halafu TPLF imetoka na kusema haina uwezo wa kushambulia shabaha iliyo umbali wa kilomita 300 tu, bali pia inaweza kushambulia mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa ambao upo umbali wa kilomita 700.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako