• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa reli mjini Nairobi kupunguza msongamano wa magari

    (GMT+08:00) 2020-11-11 10:56:00

    Nchini Kenya serikali imezindua mfumo mpana wa usafiri wa umma kusaidia kupunguza msongamano wa magari katika mji mkuu Nairobi.

    Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesema kwenye uzinduzi wa mfumo huo wa reli kwamba kutakuwa na upanuzi wa awamu kadhaa ili kufikia maeneo mengi ya mji na viunga vyake.

    Mjini Nairobi, kama miji mikuu mingi kote duniani, unazongwa na tatizo la msongamano wa magari, hasa asubuhi na jioni wakati wa pilka za kwenda kazini na kurejea nyumbani.

    Kuwepo kwa magari mengi na barabara nyembamba inamaanisha wakaazi wanatumia muda mwingi barabarani.

    Lakini sasa kufuatia kuzinduliwa kwa huduma ya usafiri wa reli, shinikizo barabarani inatajiwa kupungua.

    Mfumo huo mpya wa usafiri utawezesha wasafiri kuabiri treni hizo mpya kwenye vituo mbalimbali ambavyo pia vimeunganishwa na huduma ya mabasi ya mwendo kasi.

    Maeneo yanayonufaika moja kwa moja ni kama vile katikati mwa jiji, Kikuyu, Kitengela, Thika, Syokimau na Embakasi.

    Rais Uhuru Kenyatta anaupongeza mfumo huu wa usafiri kama wenye kuinua hadhi ya mji na uchumi kwa jumla.

    'Leo ni mwanzo mpya kwa mji wa Nairobi na viunga vyake. Kupitia juhudi hizi tunarejesha hadhi ya mji wetu mkuu na watu wake. Pia tuongeza umaarufu wetu kama lango kuu la kanda ya Afrika Mashariki na kati. Tuna kila sababu ya kujivunia mji wetu ambao sasa unaongoza kivitendo barani Afrika, kwa kuimarisha mifumo yake ya usafiri wa umma. Tunaleta suluhu za haraka kwa biashara wakati huo huo tukilinda mazingira yetu. Kwa jumla tunaboresha maisha kwa wakaazi wa Nairobi na wageni'

    Kulingana na taakwimu za mamlaka ya kitaifa ya usafiri NTSA, Mji wa Nairobi utakuwa na magari zaidi ya milioni 1.35 ifikapo mwaka 2030 na kwa wastani kila mwaka magari mapya 90,000 hununuliwa kila mwaka mjini humo.

    Na kulingana na taasisi ya maswala ya kiuchumi nchini humo, msongamano wa magari nchini Kenya husababisha kupotea kwa zaidi ya shilingi milioni 50 kila siku, sawa na dola za kimarekani 500,000.

    Uzinduzi wa mradi na mfumo huu mpya wa usafiri ni sehemu ya juhudi za serikali zinazoongozwa na jopo lililobuniwa hivi karibuni la kuboresha huduma mjini Nairobi.

    Mkurugenzi Mkuu wa huduma za jiji la Nairobi Jenerali Mohamed Badi anasema

    'Tutakuwa na maeneo kadhaa ya kuegesha magari yote ya usaifiri wa umma yanaoingia mjini Nairobi, nje kidogo ya katikati mwa mji. Kwa jumla ya takuwa maeneo 6. Tutajenga eneo kubwa la kuegesha magari ya usaifir wa umma katika mzunguko wa globe cinema kwa ajili ya magari yanayotumia barabara ya Thika. Treni nazo zitaelekea maneo yote ya Nairobi kwa mfano ile ya Embakasi ambayo huwa inajaa wasafiri kuanzia saa kumi na moja alfajiri'

    Kulingana na shirika la reli nchini humo huduma mpya ya treni itasafirisha zaidi ya watu milioni 3 kwa mwezio.

    Ili kuboresha utenda kazi, treni itasimama kwa dakika 2 tu kuwezesha abiria kushuka au kuabiri kwenye vituo mbalimbali na malipo yatafanywa kwa njia ya simu.

    Wakaazi wa Nairobi wamekaribisha huduma hii mpya.

    Kwa jumla kutakuwa na treni 11 na vituo 20 vidogo vitaongezwa ili kufikisha wasafiri karibu zaidi na wanakoenda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako