• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Ethiopia yaonya dhidi ya kampeni ya upotoshaji habari inayofanywa na TPLF

    (GMT+08:00) 2020-11-12 09:08:52

    Serikali ya Ethiopia imeonya dhidi ya kampeni kubwa ya upotoshaji habari inayofanywa na chama cha TPLF cha Tigray wakati ambapo kimeshindwa kwenye mapambano yanayoendelea na Jeshi la Ulinzi la Ethiopia.

    Akiongea na wanahabari Waziri wa Ulinzi Kenea Yadeta amesema TPLF inaeneza habari za kupotosha kwa kulishutumu jeshi la Ethiopia kuwa linalenga watu wa Tigray pamoja na miundombinu kwenye mkoa huo, wakati ukweli ni kwamba jeshi linalenga kikundi cha TPLF na wapiganaji wake. Mapema Novemba 4 serikali ya nchi hiyo imeanza kufanya operesheni ya kijeshi dhidi ya TPLF chama tawala cha mkoa wa kaskazini wa Tigray na sasa wapo kwenye vita na serikali kuu kufuatia TPLF kuripotiwa kuishambulia kamandi ya Kaskazini ya jeshi la Ulinzi la Ethiopia. Afisa mwandamizi wa jeshi la Ethiopia ameliambia Shirika la utangazaji la Fana linalomilikiwa na serikali kwamba, hadi sasa wapiganaji 550 wa TPLF wameuawa katika sehemu ya magahribi ya mkoa huo.

    Wakati huohuo Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa ripoti likisema mamia ya Waethiopia wanakimbia vita na kwenda Sudan kutafuta hifadhi katika jimbo la Gedaref.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako