• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika yatafuta msaada wa kibinadamu kwa Somalia iliyokumbwa na mafuriko

    (GMT+08:00) 2020-11-12 09:09:14

    Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na mamlaka za Sudan zimetoa wito wa kutolewa misaada ya dharura ili kusaidia maelfu ya watu waliokimbia makazi kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika sehemu kadhaa za nchi hiyo.

    Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu OCHA imesema misaada ya haraka inahitajika ili kuwezesha wafanyakazi na mamlaka za huko kutoa maji safi ya kunywa, makazi ya dharura, chakula na msaada wa vifaa ili kuondoa maji yaliyotuama ambayo yanahatarisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko. Idadi ya watu walioathirika kwenye msimu huu wa mvua imeongezeka na kufikia karibu 73,000 tangu mwezi Oktoba, wakiwemo watu zaidi ya watu 13,000 waliokimbia makazi na wanne kushukiwa kufariki.

    Shirika hilo la UM limesema majimbo matano yakiwemo Banadir, Jubaland, Hirshabelle, Galmudug na Kaskazini Magharibi yameathirika na yanaendelea kuripoti uharibifu mkubwa wa miundombinu na mashamba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako