• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC kuanzisha mkakati wa pamoja wa kulipa kodi ya uchumi wa kidijitali

    (GMT+08:00) 2020-11-12 09:09:31

    Mamlaka za kodi za nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC jana zilikubaliana kuanzisha mkakati wa pamoja wa kulipa kodi ya uchumi wa kidijitali.

    Mamlaka za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Sudan Kusini pamoja na Burundi zimesema kodi ya kidijitali inaweza kusaidia kuongeza mapato yanayohitajika kwa ajili ya kutoa huduma za umma. Pia mkakati huo wa pamoja utaweza kushughulikia msuala yanayohusiana na mwongozo wa kisheria kwa upande wa maana, utambuzi wa wahusika na mifumo ya kisheria. Nchi hizo pia zimekubaliana kufuatilia haraka mafungamano ya mifumo ya ndani ya nchi ya kodi katika kanda hiyo.

    Kwa mujibu wa maafisa wa kodi wa kanda hiyo, mamlaka zote za mapato zimeripoti kupungua kwa uingiaji wa mapato katika kipindi cha Machi hadi Septemba kutokana na janga la COVID-19 ambapo mwezi Mei ndio yalipungua zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako