• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya Marekani kutotekeleza marufuku dhidi ya TikTok ikisubiri maamuzi ya mahakama

    (GMT+08:00) 2020-11-13 17:15:53

    Wizara ya biashara ya Marekani imesema haitatekeleza amri ya kupiga marufuku app ya TikTok ili kusubiri maamuzi ya mahakama.

    Mahakama moja ya taifa imesema taarifa hiyo ya dakika za mwisho ya wizara ya biashara ilianza kutekelezwa jana.

    Taarifa imesema uamuzi wa kutotekeleza marufuku hiyo ulitolewa na Jaji tarehe 30, kufuatia kesi iliyofunguliwa na watengeneza maudhui watatu wa TikTok.

    Tarehe 6 Agosti Rais Trump alitoa amri ya Rais ya kuipiga marufuku TikTok na kampuni ya ByteDance baada ya siku 45, akitaja wasiwasi kuhusu usalama wa taifa. Amri kama hiyo pia ilitolewa dhidi ya App ya Wechat.

    Profesa Jeffrey Sachs wa Chuo Kikuu cha Columbia amekosoa uamuzi wa Rais Trump na kuutaja kuwa una lengo la kuidhoofisha China kwenye uchumi wa kidigitali, na hasa ni kwa sababu ya siasa za kijiografia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako