• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa kuhamasisha muungano wa dunia kudhibiti hewa ya ukaa kuanzia mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2020-11-13 18:52:02

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amesema umoja huo unapanga kuhamasisha muungano wa dunia kwenye kufikia lengo la kutimiza uwiano kati ya utoaji na ufyonzaji wa hewa ya ukaa (Carbon neutrality) kuanzia mwaka kesho.

    Bw. Guterres amesema haya kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu baraza la amani la Paris.

    Bw. Guterres amesema miaka mitano baada ya kupitishwa kwa Makubaliano ya Paris kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi, "bado hatuko kwenye mwelekeo unaotuwezesha kudhibiti ongezeko la joto duniani ndani ya nyuzi 1.5". Akisisitiza umuhimu wa hatua hiyo, Bw. Guterres amesema mwaka 2021 unatakiwa kufanywa kuwa "mwaka wa kupata mafanikio makubwa ya kupunguza hewa ya ukaa".

    Amesema hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka kesho, nchi zinazowakilisha asilimia 65 ya hewa ya Carbon Dioxide inayotolewa duniani, na zaidi ya asilimia 70 ya uchumi wa dunia, utakuwa umetoa ahadi kabambe ya kupunguza hewa ya ukaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako