• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchumi wa Afrika aona makubaliano ya RCEP yatailetea dunia fursa za maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-11-16 17:08:51

    Makubaliano ya Kikanda ya Uhusiano wa Washirika wa Kiuchumi wa Pande zote (RCEP) yalisainiwa rasmi jana Jumapili. Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi wa Afrika Bw. Job Ogunda amesema, makubaliano hayo yatatoa athari kubwa kwa mnyororo wa ugavi duniani, na pia yanastahili kuigwa na Afrika. .

    Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi wa Afrika na mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika Mashariki cha Taasisi ya Haki za Binadamu na Biashara (IHRB) Bw. Job Ogunda anaona kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo si kama tu kutatia moyo kwenye maendeleo ya uchumi wa kikanda, bali pia kutatoa fursa za maendeleo kwa sehemu mbalimbali za dunia, ikiwemo Afrika.

    "Kusainiwa kwa makubaliano ya RCEP kutatoa athari kubwa kwa mnyororo wa ugavi duniani, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa dunia. Makubaliano hayo pia yatapunguza kwa kiasi kikubwa vizuizi vya kibiashara, kuhimiza ongezeko la mahitaji ya soko, kuchochea shughuli za kibiashara, na kusukuma mbele maendeleo ya biashara yenye ongezeko kubwa la thamani. Makubaliano hayo si kama tu yatazinufaisha nchi za kikanda, na bali pia yataleta manufaa kwa nchi zilizoko nje ya kanda hiyo, kuhimiza mahitaji ya dunia kwa bidhaa za Afrika, na kuwaletea fursa za maendeleo."

    Bw. Ogunda amesema mpaka sasa nchi wanachama 54 wa Umoja wa Afrika wamesaini makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika, ambayo yanafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya Afrika, na kuziingiza nchi nyingi zaidi za Afrika kwenye mnyororo wa thamani wa kikanda na dunia nzima. Lakini amesema nchi za Afrika bado ziko kwenye hatua ya mwanzo, na zinahitaji kujifunza uzoefu wa kukabiliana na changamoto na kuvutia washirika wapya, hivyo kusainiwa kwa makubaliano ya RCEP kunaweka mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika.

    "Kusainiwa kwa makubaliano ya RCEP kunapaswa kuzifanya nchi za Afrika zitambue kuwa katika siku zijazo zinahitaji kufanya mazungumzo na kufikia mwafaka, ili kushirikiana katika kuhimiza maendeleo ya kikanda. Nchi za Afrika pia zinahitaji kuweka mkakati wa pamoja wa muda mrefu na kutoa vigezo vya pamoja, na kufanya kama zilivyofanya nchi za Asia, ili kujiingiza kwenye biashara ya kimataifa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako