• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IFRC: Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa zaidi kuliko COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-11-17 18:37:17

    Shirikisho la Kimataifa la Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) limeonya kuwa, mabadiliko ya tabianchi yanaleta changamoto kubwa zaidi kwa binadamu kuliko janga la virusi vya Corona.

    Katika ripoti yake, "Lije Joto au Mafuriko" iliyotolewa leo, Shirikisho hilo limesema dunia imekumbwa na majanga 100 katika miezi sita ya janga la virusi vya Corona, na zaidi ya watu milioni 50 wameathirika.

    Ripoti hiyo imesema, idadi ya majanga yanayohusiana na hali ya hewa ama mabadiliko ya tabianchi yamekuwa yakiongezeka kwa karibu asilimia 35 kila muongo mmoja tangu miaka ya 1990, na majanga haya yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 410,000 tangu mwaka 2010.

    Ripoti hiyo pia imesema, mwaka 2019 pekee, majanga 308 ya asili yalitokea duniani, na kusababisha vifo vya watu 24,400, na asilimia 77 ya majanga hayo yanahusiana na hali ya hewa ama mabadiliko ya tabianchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako