• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani amfuta kazi mkuu wa usalama wa mtandao kutokana na taarifa kuhusu usalama wa uchaguzi

    (GMT+08:00) 2020-11-18 17:01:53

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kupitia ukurasa wake wa wa Twitter kuwa, mkurugenzi wa Mamlaka ya Usalama wa Mtandao na Miundombinu ya Usalama nchini humo (CISA) Bw. Chris Krebs ameondolewa kwenye wadhifa huo kutokana na taarifa yake kuhusu usalama wa uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.

    Wakati huohuo, rais Trump amedai kuwa kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, ikiwemo watu waliokufa kupiga kura, wasimamizi wa kura kutoruhusiwa katika vituo vya kupigia kura, na hitilafu kwenye mashine za kupigia kura zilizobadili kura kutoka Trump kwenda kwa Biden.

    Wiki iliyopita, CISA ilitoa taarifa ikithibitisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 ndio ulikuwa salama zaidi katika historia ya Marekani, na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote wa kupotea kwa kura, kubadilisha kura, au vitendo vyovyote vya ukiukaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako