• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yatangaza uwekezaji mkubwa zaidi jeshini katika miaka 30

    (GMT+08:00) 2020-11-19 18:15:47

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema, nchi hiyo itaongeza bajeti yake ya ulinzi kwa dola za kimarekani bilioni 21.8 katika miaka minne ijayo, ikiwa ni bajeti kubwa zaidi ya jeshi tangu Vita ya Baridi.

    Waziri mkuu huyo amesema, amechukua uamuzi huo wakati wa janga la virusi vya Corona kwa kuwa ulinzi wa nchi ni lazima upewe kipaumbele. Amesema hali ya kimataifa ni yenye utatanishi zaidi na ushindani mkali zaidi kuliko wakati wowote tangu kumalizika kwa Vita ya Baridi, na Uingereza lazima iwe mkweli wa historia yake na kusimama pamoja na washirika wake.

    Program hiyo ambayo itafadhili miradi ya ulinzi wa mtandao na anga ya juu, inatarajiwa kutoa nafasi 40,000 za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako