• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la kiserikali la Marekani laruhusu kipindi cha mpito wa urais cha Biden

    (GMT+08:00) 2020-11-24 18:17:00

    Shirika la Usimamizi wa Huduma za Jumla la Marekani GSA jana lilimwambia Joe Biden liko tayari kuanza mchakato rasmi wa kipindi cha mpito wa urais kwa ajili yake.

    Kwenye barua yake kwa Biden, Msimamizi mkuu wa GSA Emily Murphy amesema amejiandaa kuhakikisha rasilimali na huduma baada ya uchaguzi zinapatikana kwa ajili ya kipindi cha mpito cha Biden kuingia ikulu ya White House, na kusisitiza kwamba licha ya matukio ya karibuni yanayohusisha changamoto za kisheria na uthibitisho wa matokeo ya uchaguzi, ametoa maamuzi yeye mwenyewe, kulingana na sheria na ukweli uliopo.

    Jumatatu hiyohiyo rais Donald Trump naye aliandika kwenye Twitter kwamba ameipa mapendekezo GSA kufanya kile kinachohitajika kufanywa kuhusiana na itifaki za awali, na kwamba ameielekeza timu yake kurahisisha mpito wa Biden ingawa hadi leo bado hajakubali kushindwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako