• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya

  • Ardhi oevu ya mto Huanghe mjini Zhengzhou ni moja ya njia nane za uhamiaji wa ndege duniani.

    Njiwa wakiruka kwenye uwanja wa Lvcheng, ambao ni alama ya amani na neema kwa wakazi wa huko

    Wilaya ya Zhongyuan wakati wa usiku

    Hewa safi imeongezea zaidi mvuto wa mji huu. Picha hii imepigwa katika mtaa wa makazi ya Dihu, wilayani Zhongyuan.

    Jumba la makumbusho la mji wa Zhengzhou likionyesha utamaduni wa miaka maelfu kadhaa katika uwanda wa kati wa China.

    Kampuni ya kutengeneza mashine zinazotumika kwenye uchimbaji wa makaa ya mawe ya Zhengzhou ZMJ ilitengeneza mashine ya kwanza ya hydraulic support nchini China, bidhaa zake zinatumika katika kampuni za kuchimba madini kote nchini China, na pia zinauzwa Russia, India na Uturuki

    Wilaya ya Zhongyuan yapendeza sana wakati wa usiku hususan siku za sikukuu.

    Jumba la sayansi na teknolojia la Zhengzhou lililoko wilaya ya Zhongyuan lavutia zaidi wakati wa usiku.

    Mlima Songshan, moja ya milimu maarufu nchini China.

    Maonyesho ya muziki na Kongfu ya Shaolin, ambayo ni maonyesho pekee yanayofanyika katika mazingira halisi ya kimaumbile kwenye sehemu ya kaskazini mwa China.

    Jumba jipya la maktaba mjini Zhengzhou.

    Mnara wa kumbukumbu ya mgomo mkubwa wa wafanyakazi wa reli ya kutoka Beijing hadi Wuhan uliofanyika Februari 7 mwaka 1923, ambao ni moja ya majengo maarufu mjini Zhengzhou.

    Daraja la kupita magari na treni kwenye mto wa Huanghe mjini Zhengzhou, ambalo ni refu zaidi la aina hiyo duniani.

    Eneo la kusubiri ndege kwenye uwanja wa ndege wa Xinzheng mjini Zhengzhou.

    Kituo cha treni ya mwendo kasi Mashariki mwa mji wa Zhengzhou

    Ushoroba wa kijani wenye urefu wa kilomita 500 wajengwa mjini Zhengzhou.

    Wilaya mpya ya Zhengdong iliyoanzishwa miaka ya karibuni katika mji wa Zhengzhou.

    Kituo cha sanaa cha mji wa Zhengzhou wakati wa usiku

    Mwanga wa mwezi kwenye mlima wa Songshan

    Maonesho ya Kungfu yaliyoshirikisha wanafunzi elfu 10 wa shule ya Kungfu ya Tagou

    Mnara wa hekalu la Songshan unavyoonekana kutokea mbali

    Mnara wa hekalu la Songyue, ulioko ndani ya hekalu la Songyue kilomita 5 kaskazini magharibi mwa mji wa Dengfeng mkoani Henan, ulijengwa miaka 1470 iliyopita. Mnara huu ni wa kale zaidi nchini China ambao ulijengwa kwa matofali.

    Bahari ya mawingu kwenye mlima Songshan

    Tamasha la Kongfu ya Shaolin

    Eneo la minara ya kuhifadhia majivu ya watawa wakubwa wa dini ya budha kwenye hekalu la Shaolin

    Kongfu ya Shaolin

    Shamrashamra za sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa Kichina.

    Ushoroba wa kijani ukionekana mahali popote mjini Zhengzhou

    Utamaduni wa Mto Huanghe

    Ardhi oevu ya Mto Huanghe

    Wachina watokao sehemu mbalimbali duniani wakikusanyika kutoa heshima kwa Huangdi, ambaye ni mmoja wa mababu wa kale wa Wachina. Sherehe hiyo hufanyika huko Xinzheng mkoani Henan, ambako ni maskani ya Huangdi, kila tarehe 3 mwezi wa 3 katika kalenda ya kilimo ya Kichina, ambayo ni siku ya kuzaliwa ya Huangdi.

    Taige, sanaa ya jadi ya mkoa wa Henan

    Guan Xing Tai, jengo la ghorofa la kutafitia nyota lililojengwa na mwanafalaki wa enzi ya Yuan ya China Bw. Guo Shoujing (1231B.K.-1361B.K.), ni mahali pa kale zaidi pa kutazama nyota nchini China, pia ni moja la majengo maarufu ya sayansi ya falaki duniani, na lina umuhimu mkubwa katika historia ya falaki na ya ujenzi.

    Ufunguzi wa tamasha la 10 la sanaa za Asia ukifanyika mjini Zhengzhou

    Maonyesho ya muziki na Kongfu yanayoonyesha utamaduni wa kibudhaa wa hekalu la Shaolin

    Maonyesho ya fashfash ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China mwaka 2010 kwenye wilaya mpya ya Zhengdong

    Tembelea wilaya mpya ya Zhengdong iliyoanzishwa miaka ya karibuni katika mashariki mwa mji wa Zhengzhou
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako