• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Krismas mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2009-12-29 10:35:01

    Pamoja na kuwa Beijing is mji wenye wakristo wengi kama ilivyo kwenye miji mikuu ya nchi za Afrika na za Magharibi, hali ya shamrashamra ya sikukuu ya Krismas ni rahisi kuonekana mjini Beijing.

    Mbali na supamaketi na maduka makubwa kuwa na mapambo ya Santa Klauss, miti ya Krismas na hata nyimbo za Krismas, klabu mbalimbali pia ziliandaa sherehe kwa ajili ya mkesha wa krismas na sikukuu ya Krismas.

    Kwa kuwa Beijing ni kama nyumbani kwa watu kutoka kila kona ya dunia, watu kutoka sehemu mbalimbali na wenyeji wao walijumuika kwenye klabu mbalimbali kusherehekea mkesha na siku ya krismas. Mimi nilibahatika kutembelea Klabu mbili, moja wakati wa mkesha na nyingine siku ya krismas. Kwenye mkesha wa Krismas niliona vijana wengi wenyeji kwa wageni wakijumuika kwenye Klabu ya Chambers ambayo DJ mtanzania Bw Moses aliendesha sherehe na kutoa burudani safi ya muziki. Na kwenye Klabu nyingine bendi moja ya wachina, waafrika na watu kutoka Ulaya ilitoa burudani safi kwa watu waliofika kwenye klabu hiyo. Kwa ujumla Krismas kwa upande wa burudani ilikuwa nzuri sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako