• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kusherehekea sikukuu ya Krismas pamoja na Dj Mosy

    (GMT+08:00) 2009-12-29 16:01:53

    Kipindi hiki ni cha nne katika mfululizo wa vipindi vya "Fuatana nami, ione Beijing", katika vipindi vilivyopita tumefuatana na Bw. Fadhili Mpunji kuona kundi la vijana wa China jinsi wanavyopiga ngoma, kupanda subway ya Beijing na kutembelea sehemu ya Nanluoguxiang. Katika kipindi hiki, Bw. Fadhili atatuonesha jinsi wachina wanavyosherehekea sikukuu ya Krismas.

    Kwa kuwa mara nyingi Bw. Fadhili anakuwa na pilika pilika za kazi, kwa hivyo hana nafasi kubwa ya kuonana na marafiki zake. Katika siku ya Krismas, alipata mapumziko na kuamua kumtembelea mtanzania mwenzake Bw. Emanuel Mosy Onasaa.

    Bw. Mosy ni mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania. miaka minne iliyopita alikuja hapa Beijing, China kuanza masomo yake ya kozi ya uchumi wa kimataifa na biashara katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Beijing. Baada ya kuishi kwa miaka minne nchini China, amekuwa nusu ya mchina.

    Bw. Mosy anapenda sana sanaa, anajua jinsi ya kucheza ngoma na kuchora picha za aina mbalimbali, na aliwahi kuonesha sanaa ya Afrika kwenye sherehe ya sikukuu ya Spring kwenye bustani ya Chaoyang hapa Beijing. Mbali na hayo, Bw. Mosy anapenda sana muziki wa aina mbalimbali, kwa kuwa ameishi kwa muda mrefu hapa Beijing, hivyo anafahamu sifa ya nyimbo za kichina. Pia anajua namna ya kufanya kazi ya DJ, baada ya masomo huenda kufanya kazi ya DJ kwenye club mbalimbali za sehemu ya Wudaokou, na muziki anaouchagua unakaribishwa sana na mashabiki wa muziki wa China na wa nchi za nje.

    Siku ya mkesha wa Krismas, alifanya kazi ya DJ kwenye club inayoitwa Chamber iliyoko katika sehemu ya Wudaokou. Pia alimwalika mwenzake Bw. Fadhili kwenda kushiriki kwenye sherehe hiyo. Sherehe hiyo ilianza saa nne usiku, ambapo Bw. Mosy alianza kupiga muziki. Baada ya nusu saa hivi, vijana wengi walijaa kwenye ukumbi wa Chamber Club, walikunywa vinywaji, kucheza dansi na kuburudika na muziki. Kila mmoja alikuwa na furaha sana.

    Bibi Wang Dongdong ni kijana anayefanya kazi katika kampuni ya nchi za nje, siku hiyo pia alikwenda kwenye Club hiyo kushiriki kwenye sherehe hiyo. Bibi Wang alisema kwa kawaida ana kazi nyingi kila siku, hivyo hana nafasi kubwa ya kujiburudisha. Na sikukuu hiyo ni fursa nzuri kwake kupata mapumziko. Pia anapenda sana muziki hasa nyimbo za Afrika zilizopigwa na DJ Mosy.

    Miaka ya hivi karibuni, vijana wengi zaidi wameanza kusherehekea sikukuu ya Krismas kwa njia mbalimbali. Tuna imani kuwa kama utakuja hapa China katika sikukuu ya Krismas, hutaona uchovu na utasherehekea sikukuu hiyo pamoja na wachina wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako