• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uholanzi yaiona hatua ya fainali baada ya miaka 32

    (GMT+08:00) 2010-07-07 10:50:39

    Baada ya miaka 32 sasa Uholanzi imekuwa timu ambayo inatinga tena kwenye hatua ya fainali kwa kuichabanga Uruguay kwa magoli 3 kwa 2. Mchezo huo uliotawaliwa na kadi za njano 5, ulianza kwa kasi ya ajabu hasa kwa upande wa Uholanzi ambao ndio walionekana kuumiliki mpira zaidi.

    Goli la kwanza ambalo lilikuwa la kushtukiza na kufungwa kutoka mbali na kepteni wa timu ya Uholanzi Van Bronkhorst katika dakika ya 18, liliwaduwaza wachezaji wa timu ya Uruguay ambao awali walijitapa kuwa ulaya hakuna timu inayowatisha. Na katika dakika ya 40 kipindi hichohicho cha kwanza kepteni wa timu ya Uruguay Diego Forlan alirudisha majibu kwa kuipatia Uruguay goli la kwanza ambalo nalo pia lilifungwa kutoka mbali, na mapaka mapumziko timu hizo zilikuwa na sare ya 1kwa 1.

    Katika kipindi cha pili uholanzi ilicharuka kwa kuibandika Uruguay magoli mawili mfululizo yaliyopishana kwa dakika tatu tu, ambapo katika dakika ya 70 mchezaji Wesley Sneijder aliipatia timu yake goli la pili na la tatu kumaliziwa na Arjen Robben.

    Mara ya mwisho kabisa uholanzi kufikia hatua ya fainali ilikuwa mwaka 1978 ambapo walipoteza mchezo kwa Argentina ambao ndio waliokuwa wenyeji wa michuano ya mwaka huo.

    Sasa uholanzi inatarajia kucheza na Ujerumani au Hispania siku ya jumapili baada ya kujulikana mshindi katika mechi itakayochezwa leo saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako