Goli la ufundi lililofungwa kwa kichwa na mchezaji Carles Puyol katika dakika ya 73, limeifanya Hispania kwa mara ya kwanza itimize ndoto yake ya kufika hatua ya fainali, kwenye michuano ya kombe la dunia. Mshambuliaji huyo wa Hispania aliibuka na kuifungia timu yake goli pekee ambalo litakumbukwa daima na mashabiki wa soka hasa wa Hispania.
Ujerumani nayo kwa upande wake haikuonesha soka nzuri, kwani walizidiwa nguvu tangu dakika ya mwanzo, jambo ambalo liliwanya washindwe hata kufurukuta mbele ya Hispania, hili ni pigo jingine kwa ujerumani baada ya lile la mwaka 2008 kwenye michuano ya ulaya ambapo ujerumani ilibanjuliwa kwa bao 1-0 na kuwafanya Hispania wavikwe taji la ulaya . Wakati ujerumani inacheza nusu fainali kwa mara ya 12, Hispania wao ni mara yao ya kwanza.
Sasa ujerumani itacheza na Uruguay siku ya jumamosi katika mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu, ambapo Hispania itavaana na uholanzi katika mechi ya fainali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |