
Timu ya Ujerumani imefanya kile ilichotarajiwa na wengi baada ya kuichabanga timu ya Uruguay kwa magoli matatu kwa mawili. Ujerumani ilifunga goli la kwanza katika dakika ya 19 goli lililofungwa na mshambuliaji Muller, na Uruguay ilisawazisha dakika 9 baadaye kupitia mshambuliaji wake Edinson Cavan. Na katika dakika ya 51 mfungaji hatari Diego Forlan alifungia goli timu Uruguay na kuongoza hadi dakika ya 56 wakati Marcel Jansen alipoisawazishia Ujerumani katika dakika ya 56. Sami Khedira wa Ujerumani alifungia timu yake goli la ushindi katika dakika ya 82, na kuifanya Ujerumani ichukue nafasi ya tatu kwenye kombe la dunia.