Touchroad International Holdings Group (Touchroad Group) ni kampuni inayojihusisha na uendelezaji wa hifadhi, utafiti wa madini,ufumaji wa nguo,biashara ya kimataifa na utalii barani Afrika.
Biashara za kampuni hili zilianzia Ghana mwaka 2000 isipokuwa kampuni ya Touchroad ilizinduliwa nchini China na ina uhusiano na nchi zaidi ya 25 barani Afrika,ina ofisi 8 katika nchi za kiafrika na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 600 wa kiafrika. .Mtaji wake wa uwekezaji katika nchi za kiafrika unazidi dola millioni 100 za kimarekani.
Kampuni hili lina upendo wa dhati kwa AFRIKA kwani limekuwa likijishughulisha na maendeleo ya kiuchumi ya Afrika na kumekuwa na matokeo mazuri kijamii na kiuchumi.. Touchroad Group linaamini kuwa dunia inapaswa kutoa kipaumbele kwa nchi za kiafrika.Afrika haihitaji biashara tu bali pia ufumaji wa kienyeji,viwanda vya kisasa na uchumi ilio mpana zaidi..Kampuni ya Touchroad lilianza na biashara kadhaa lakini likabadili muundo wake na kuanza kujenga viwanda vya nguo barani Afrika hivyo kuondokana na nguo zilizotengenezwa China na kuanza kutengeneza nguo hukohuko Afrika. Touchroad limetengeneza mazingira mazuri ya ajira kwa waafrika wakati huohuo limetengeneza hifadhi nchini Botswana, ambayo itawavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini humo hivyo kutoa ajira zaidi na kueneza teknolojia hiyo.
Wakati wa msukosuko wa fedha duniani makampuni mengi ya nchi za magharibi yalipata shida katika kuendesha shughuli zake barani Afrika lakini cha ajabu kampuni hii badala ya kupunguza wafanyakazi iliajiri watu wengi zaidi hivyo kupunguza tatizo la ajira. Touchroad imesifiwa sana kwa hili na serikali husika na watu wake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |