Shirika la uchimbaji wa mafuta la China (CNOOC) ni moja ya makampuni makubwa yanayomilikiwa na serikali ya China. Jukumu lake kubwa ni kuendeleza raslimali za majini kwa ushirikiano na wabia wa nje. Kampuni hii iliyoanzishwa mwaka 1982, inajihusisha na maeneo sita ambayo ni utafutaji wa mafuta na gesi, usafishaji wa mafuta na utengenezaji wa mbolea, gesi na umeme, nishati mpya, huduma za kiufundi, na huduma za fedha.
Kutokana na mtazamao wake wa maendeleo ya kisayansi na kuhuimizwa na lengo la kutaka kuwa moja ya makampuni makubwa ya nishati duniani, CNOOC imekuwa ikitekeleza mikakati minne ya "maendeleo yaliyopangwa, human-based revitalization, teknolojia zinazoongoza, na gharama nafuu", na imepata "mafanikio manne makubwa" kwenye utafutaji wa mafuta na gesi, kutoka mwanzo wa mkondo, katikati hadi mwisho wa mkondo, kutoka kwenye kina kifupi na kwenye kina kirefu, na kutoka nyumbani na ng'ambo, na kutoka nishati za jadi hadi kwenye mseto wa nishati za jadi na nishati mpya. Hivi sasa CNOOC imekuwa kampuni ya kisasa yenye uwezo kiasi wa ushindani na nguvu ya ushawishi duniani.
Mwaka 2009 Kampuni ya CNOOC ilizalisha tani milioni 47.66 za mafuta, likiwa ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, na ilizalisha bidhaa za mafuta zenye tani milioni 32. Mapato yake yalifikia Yuan bilioni 209.6, huku faida yake baada ya kodi na makato ikifikia Yuan bilioni 52.4, na kodi na iliyolipa ilikuwa Yuan bilioni 50.7. Thamani ya mali za kampuni imefikia Yuan bilioni 518.3, thamani halisi ikiwa ni Yuan bilioni 325.5. Jarida la Fortune liliichagua kampuni hiyo kuwa ya 318 kati ya makampuni 500 makubwa duniani.
CNOOC ina shughuli nyingi barani Afrika, lakini imewekeza zaidi nchini Nigeria. Kampuni hiyo inamiliki asilimia 45 ya faida kwenye kitalu namba OML nchini Nigeria. Mradi huo wa uchimbaji kwenye kina kirefu una maeneo sita yenye mafuta AKPO, EGINA, EGINA South na PREOWEL. Eneo la ARKO lilianza kazi mwezi machi 2009. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2009, CNOOC ilikuwa imechimba visima 24. Mbali na Nigeria, kampuni pia ina hisa kwenye baadhi ya vitalu nchini Kenya, Guinea ya Ikweta, Jamhuri ya Kongo na Libya. Vitalu hivyo kwa sasa viko kwenye hatua ya utafutaji wa mafuta.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |