Kwa wanaotoka Tanzania na Zambia wanajua sana umuhimu wa urafiki baina ya China na Africa hasa kutokana na Reli ya Tazara ambayo hadi leo inatumiwa na nchi mbili hizo na imekuwa ni kichocheo kikubwa cha maendelea kwa wananchi wa nchi hizo.
Reli ya Tazara ilijengwa miaka mingi iliyopita, lakini bado inafanya kazi hadi leo, na ilijengwa kwa msaada wa serikali ya China ili kuzisaidia Tanzania na Zambia kurahisisha mawasiliano kati yao, na pia imekuwa chachu ya maendeleo kwa nchi hizo.
Wananchi wa Tanzania na Zambia wamekuwa wakisafiri kirahisi kwa kutumia Reli hiyo toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na hata ndani ya nchi hizo wananchi wake wamekuwa wakitumia rel hiyo kwa safari mbali mbali.
Reli hiyo haizinufaishi Tanzania na Zambia tu, bali hata nchi za jirani kama Malawi na Congo DRC nazo zimekuwa zikinufaika na Reli hiyo hasa kibiashara kutokana na kusafirisha bidhaa zao toka aidha Tanzania au Zambia kwenda kwenye nchi zao.
China imefanya mambo mengi sana kwenye nchi mbali mbali za Africa, na hivi sasa China inachukuliwa kama mkombozi wa bara hilo katika harakati za kuleta maendeleo kutokana na uwekezaji pamoja na shughuli mbali mbali za maendeleo. Hivi sasa kuna makampuni mengi ya Kichina barani Afrika yakifanya kazi mbali mbali kama vile ujenzi wa barabara.
Kwa mie ninaetoka Tanzania, China imefanya mambo mengi nchini kwetu. Ukiacha Reli ya Tazara, kuna kiwanda cha nguo cha Urafiki ambacho kilikuwa kinafanya kazi kwa ushirikiano wa Tanzania na China. Na kwa wale wapenda mpira wa miguu, kwao China ndio usiseme kabisa, maana ukitaja tu nchi hiyo basi unataja uwanja mkubwa wa soka uliopo jijini Dar es salaam uliojengwa na serikali ya China wenye uwezo wa kubeba watu elfu 60 kwa wakati mmoja.
Uwanja huo umekuwa kivutio kikubwa mno kwa soka la Tanzania, na umeanza kuleta faida hasa kutokana na timu kubwa kubwa kucheza na timu za Tanzania. Ninakumbuka nyota wa soka maarufu duniani kama Samweli Eto`o wa Cameroon, Ricardo Kaka wa Brazil na Didier Drogba wote
wamecheza kwenye uwanja huo na walipouona kwa mara ya kwanza, hawakuamini kama upo nchini Tanzania na yote hiyo ni kwasababu ya serikali ya China.
Si Tanzania tu iliyonufaika kwa kujengewa uwanja mkubwa wa michezo. Zipo pia nchi nyingine barani Afrika nazo zimepata masaada kama huo toka kwa serikali ya China, hivyo bado ninasema China ni muhimu mno kwa Africa.
Unapozungumzia suala la teknlojia hivi sasa barani Africa, basi China haiku mbali, kwani hivi sasa ndio inayolibeba bara hilo kwenye maswala ya teknojia, kuanzia kwenye simu za mkononi hadi kwenye kompyuta. Karibu watumiaji wengi wa simu za mkononi barani humo wanatumia simu toka China, hii inatokana na unafuu wa bei, hivyo wananchi wengi wa Africa wanazimudu bila wasiwasi wowote ule. Pia kutokana na uwekezaji wa makampuni mbalimbali ya China barani Afrika, tatizo la ajira limepungua kwa kiaso kikubwa, na hivyo kuwa chachu ya maendeleo barani humo.
Upande wa biashara, China imekuwa soko kubwa sana kwa wafanyabiashara kutoka barani Afrika kuja kufanya manunuzi ya bidhaa zao mbali mbali. Hii inatokana na sera ya China ya kufungua mlango ambayo inawawezesha wafanyabiashara kutoka Afrika kununua bidhaa bora bila vizuizi vyovyote vile.
Mwisho kabisa, tunaomba urafiki huo baina ya China na Africa uendele kudumu maana umekuwa wa manufaa kwa pande zote mbili, na umesaidia katika kuendeleza uchumi na kuleta maendeleo barani Afrika.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |