Na sio hivyo tu kutamka hata wageni wanaokuja kufanya kazi hapa au kusoma basi majina yao yanatafsiliwa kwa lugha ya Kichina ili kuleta urahisi kwa wazawa kumjua rahisi muhusika hilo nimelipenda.
Kwa mfano nchi yangu ya asili ya Tanzania kwa kichina inaitwa TANSANIA na ukitamka wewe unavyojua eti Tanzania basi atakulekebisha tu kuwa itamkwa TANSANIA.
Sio Tanzania tu nchi karibu zote na mije yake hapa China inatamkwa kwa kichina hilo nimelipenda na ninasema kweli ni la kuigwa kwa nchi kama zetu zinazokabiliwa na kupotea kwa tamaduni zake na kurusu tamaduni za kigeni kuingia kwetu.
sie wengine ndio usiseme tumeshapewa majina ya kichina ikiwa ni tafsili ya majina yetu kwa lugha yao na ukikata mitaa wakikuliza unaitwa nani basi wewe unalitaja hilo jina lako la kichina ni majina mazuri na yanavutia.
Kwa kila anaekuja China kwa mara kwanza atalishanga sana hili na kuliona ni la ajabu ila hata nyumbani Tanzania kuna baadhi ya vitu vingine vimebadilishawa na kutamkwa kwa Kiswahili kwa mfano wa baadhi ya nchi zinatamkwa kwa Kiswahili,kwa mfano United Kingdom inayoitwa Uingereza na kwa kichina inaitwa Yingguo,German inayoitwa Ujerumani kwa Kiswahili wakati kwa Kichina inaitwa Deguo na USA inayoitwa Marekani kwa Kiswahili wakati wao china wao wenyewe wanaita Meiguo hata China yenyewe haitwi hivyo kwa kichina bali inaitwa Zhonggu
Basi hadi raha maana ujue kabisa ukitua hapa China ujue fika kuwa kila kitu kinaitwa kwa kichina na ujiandae kwa hilo ingawa mwanzoni inakuwa tabu ila ukizoea hakuna tabu safi tu.
Mwalimu mmoja wa lugha ya kichina anaeitwa Qu au Jerry anasema hilo linafanyika kuwapa uwepesi wao wachina kwenye kutamka kwa lugha yao ya asili na hawataki kuiga vitu.
Kuhusu kupewa majina ya kichina mwalimu huyo anasema hilo nalo wanalifanya ili kuwafanya wanafunzi wao wajione wapo China na kuwapa urahisi zaidi kwa kuijileza zaidi kwenye jamii ya Kichina ambayo tayari imezoea kuona kila kitu ni cha kwao tu.
Mwalimu huyo anasema hakuna ugumu wowote wa kumpa mwanafunzi jina la kichina kwasababu pale inatamfutwa tafsili ya jina lake tu ila anakili awali inakuwa ngumu kwa mwanafunzi kulikubali jina analopewa la kichina ila wakizoea inakuwa rahisi kwao.
Kingine anasema wanafunzi wao wanatoka karibu dunia nzima na wengine wanakuwa na majina magumu mno kutamka sio kwa walimu tu hata kwa wanafunzi wenzao ila majina wanayowapa wao ya kichina yanawarahisishia pia wanafunzi hao wenyewe kwa wenyewe kwenye maisha ya kila siku.
Kijana mmoja toka nchini Mali anaeitwa Amadu Keita kwa kichina anaitwa Madou anaesoma kwenye mjii wa Wuhan kati kati ya China anasema yeye anafurahia sana hilo jina ingawa awali haikuwa rahisi kwake kulikubali lakini hivi sasa safi tu na hakuna tabu pia anasema imemrahisishia kazi kwa kila kitu hapa China maana akitamka tu Madou basi wanamulewa zaidi hakuna tatizo.
Anaendelea kusema kwenye darasa lao walilokuwa wakisoma lugha ya kichina kwa mwaka mmoja karibu wote walikuwa wakijuana kwa majina ya kichina na anakili kuwa kuna baadhi ya hadi wanamaliza masomo yao ya lugha ya Kichina alikuwa hawajui majina yao ya asili ya toka kwenye nchi zao hata yeye baadhi yao walikuwa hawajui kama anaitwa Amadu Keita na hata kama akiitwa hilo jina basi inachukua muda kuelewa kama yeye kwa maana hivi sasa jina la Madou limechukua hatamu kwake.
Asikuambie mtu inaleta mvuto sio mchezo ukimkuta mchina mwenyewe akitamka hayo majina tena kwa rafudhi yake ya mjii wake wa asili yaani kama wa Wuhan au Nanchang akatamka kwa rafudhi hiyo inapendeza sana katika hilo ninawapa wachina heko.
Kikubwa hapo cha kujifunzi ni kwamba wenzetu wanapenda vya kwao na hawataki kuiga na wapo makini kusimama kutetea vitu vyao vya asili na kutangaza utamaduni wao.
Mwanafunzi mmoja wa kichina anaesoma chuo kikuu cha Nanchang anaeitwa kwa jina la Wang anasema anafurahi sana kuona mgeni anapoitwa jina la Kichina maana hata kama akirudi kwao ataenda kuelezea China na hapo tayari atakuwa ameitangaza China.
Na kitu kingine anasema anafurahiswa na kuona wageni wakiongea lugha yao ambayo anasema ipo siku itakuja kuwa lugha kubwa tu duniani kama zilivyo lugha zingine.
Na ni kweli wachina wanafurahi sana wanapomuona mgeni anaongea lugha yao na wapo tayari hata kukusaidia pale unapohitaji msaada wa kuijua lugha hiyo,hilo linanikumbusha kule Wuhan wakati ninajifunza lugha ya Kichina ambapo hata ukienda dukani ukamuuliza muuza duka kuhusu neno na maana yake au linatamkwa vipi basi bila wasi wasi wowote wala kupoteza muda anakusaidia.
Na asikuambie mtu pamoja na kujifunza lugha ya kichina darasani sehemu ya kwenda kupatia uzoefu wa kuongea hiyo lugha ni mtaani kama vile sokoni au dukani na wahusika huko ni wananchi wa kawaida na wapo tayari kukusaidia hawana roho mbaya katika kumsaidia mtu.
Kabla ya sijaondoka ngoja nikuambie katika swala la kupeana majina sio wao tu wachina wanaowapa majina wageni hata kuna baadhi ya wachina nao wamejikuta wakipewa majina na wageni wachina hao ni hasa wale wanauza maduka au sokoni wanaouza vyakula.
Ninakumbuka mama mmoja kule Wuhan anaeuza vitu sokoni amebatizwa jina la mama Said na wanafunzi wa Kitanzania huku kijana mmoja anaeuza duka akipewa jina la Masanja ambalo nalo ni jina la Kitanzania na dada mwingine akipewa jina la Mwajua yeye anauza chakula pia huko huko kwenye mjii wa Wuhan.
Hii ndio China na kila kitu ni kwa kichina china tu na nikuambie kuna raha yake ukikijua kuongea hiki kichina au kutamka majina ya vitu au mijii kwa kichina kama wanavyotamka wao wenyewe.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |