• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapenzi

    (GMT+08:00) 2011-11-22 18:12:05
    Kuna msemo katika vitabu vya dini usemao binadamu tumeletwa ilituijaze duniani, kuifanya ipendeze na yenye mvuto kila wakati, na pia kuna msemo wa wahenga usemao duniani wawili wawili ukiwa na maana kuwa mwanaume anpofikia umri Fulani anahitajika kuoa na mwanamke kadhalika aolewe.

    Usishangae msomaji wangu kwanini leo kwenye MAISHA YA UGHAIBUNI nimeanza hivi yote hii ni kuweza kukueleza hali ilivyo huku ughaibuni, ambapo wageni wengi walioko huku wameacha wake au waume zao ama wachumba au kwa Tanzania wanasema wameacha mademu zao.

    Hivyo leo langu ni kuangalia kama walio katika ndoa wapo makini na ndo zao ingawa wapo huku ughaibuni hilo ndio kubwa leo hii na ndio tunaloliangalia kwa kina hapa.

    Baadhi wanaendelea na mahusiano yao ya huko walikotoka, ilhali wengine wanaingia kwenye mahusiano mapya na kusaliti wenza wao waliowaacha nchini kwao, Ninakumbuka wakati tu nimefika nchini China mwezi Septemba 2010, rafiki yangu mmoja aliniambia ameondoka nchini akiwa kakorofishana na girlfiriend wake, baada ya wiki chache nilimuuliza endapo wamemetatua mzozo baina yao alinijibu tu kuwa hamuhitaji tena, inauma sana, na nilipomuuliza kwanini ameamua hivyo alitojibu moja tu kuwa hana mpango wa kurudi nyumbani kwa miaka mitatu mfurulizo hivyo hawezi kumpotezea muda, hadithi ikaisha hapo jamaa akaondoka zake na kuniaga kwa lugha ya kichina Zaijian (bye, ama kwaheri) Huo ni utangulizi wa mada yetu leo hii.

    Unajua katika harakati za kulinda mahusiano hasa ya mbali teknolojia hivi sasa imesaidia sana sio kama zama za miaka ya 47, hivi sasa kuna vitu kama simu za mkononi,email(barua pepe) na kuzungumza kwenye mitandao kama facebook,yahoo messenger, qq,twiter na mingineyo, pia kuna simu za bure kwenye internet ambazo mnaweza kuonana kwa sura kama skype zimesaidia kulinda mahusiano kwa kiasi kikubwa sana.

    Bibie Shanana kutoka Zanzibar mitaa ya Fuoni aliekaa kwenye ndoa kwa kipindi cha miezi miwili tu kabla ya kumuacha mumewe Mohamed na kuja nchini China kusoma anasema maisha ni magumu mno kuishi bila ya mwenza wake ambae hivi sasa anaishia kuisikia sauti tu kwenye simu au kusoma email toka kwake ama ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi.

    Msomaji wangu kitu kikubwa huku China kinachowakumba wanandoa au wapenzi waishio nchi tofauti ni masaa china iko mbele kwa masaa matano dhidi ya Tanzania, mawasiliano kwa wanandoa au wapenzi kwa nchi hizi ni kama bahatinasibu karibu kila kukicha maana inabidi kubahatisha ukipiga simu au sms inakubidi uende na mahesabu kwa mfano huku China saa mbili asubuhi huko tanzania ni saa nane usiku hapo usipokuwa makini kila mmoja anaweza kumdhania mwenzie si muaminifu kwa kuwa unaweza piga simu kumbe mwenzio kalala ni usiku mkubwa huko aliko.

    Rodney (ama Chenru kwa Kichina) toka Malawi yeye ni mwanafunzi hapa China kwenye mji wa Wuhan anasema huchukua muda mwingi sana kuongea na mchumba wake ambae nae yupo nje ya nchi yao ya asili, anasema baadhi ya nchi gharama za mawasiliano ni rahisi nasehemu nyingine ni ngumu sana. ila teknolojia imemsaidia sana ambapo imefikia kipindi huongea wakiwa wanaonana kupitia simu za video ila anakiri hiyo haikidhi hata kidogo, Chenru anaenda mbali na kusema kama mnamapenzi ya dhati hamuwezi kusalitiana hata kidogo na anaamini hivyo ila anakiri kuna wanaofanya hivyo hapa China ambao wamejiingiza kwenye mapenzi mapya wakati wameacha wachumba zao hukowatokako.

    Ila yote hayo, husababishwa na tamaa pamoja na kutokuwa na uvumilivu au kama dada yangu Johari Mayoka anaye fanyakazi katika Idhaa ya Kiswahili Radio China kimataifa anavyopenda kusema kutokuwa na ustahamilivu na kuendekeza matamanio ya mwili, na kuangukia kwenye mahusiano na walimwengu wa huku ughaibuni, Kauli hiyo inaungwa mkono na kijana Timo kutoka kusini mwa bara la Afrika, ambae ni mwanafuzi wa chuo kimoja hapa China, ambae anasema yeye binafsi ana mpenzi huko nchini kwao ila hapa China tayari ameshaingia kwenye mapenzi mapya.

    Namalizia tu kwakusema kuna changamoto nyingi huku ughaibuni hasa mfumo wa maisha yenyewe, maeneo ya starehe ni mengi na huru, pia uhuru wanaoupata huku tofauti na wanakotoka hasa kwa nchi yangu ya Tanzania maana vijana wengi wanaokuja huku kusoma wanakuwa bado wadogo na wanatoka kwenye familia zao za baba na mama.

    Hayo ndio mambo ya mapenzi huku ughaibuni maana wengine wanavumilia kama akina sie maana tunajua ipo siku tutakuwa tena pamoja na akina Mama Nancy na hatuwezi kusaliti mahusiano yetu ila wengine ndio hivyo uzalendo unawashinda na kuangukia kwenye usaliti.

    Kusema kweli inahitaji moyo wa dhati na uvumilivu wa kutosha maana kuna mengi yanajili huku Ughaibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako