• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Elimu ya China

    (GMT+08:00) 2011-11-23 15:40:21
    Waswahili wanasema, usicheze na elimu maana ndio mkombozi wako siku za baadae. Ni kweli, elimu imewakomboa wengi hapa duniani. Kwa kuzingatia hilo, CHINA imeamua kulisaidia bara la AFRICA katika suala la elimu.

    Hivi sasa hapa nchini China kuna maelfu ya wanafunzi toka pande zote za bara la AFRICA wanaosomea fani mbalimbali kwenye vyuo vikuu katika nchi hii ya mashariki ya mbali. Wengi wa wanafunzi hawa inawabidi kwanza wajifunze lugha ya kichina ambayo huko barani Africa inaaminika kuwa lugha ngumu zaidi kuwahi kutokea hapa Duniani. Na asilimia kubwa ya wanafunzi hao wanasoma kwa kudhaminiwa na serikali ya China.

    Msaada huo haujanza leo wala juzi, bali ni wa siku nyingi na umekuwa ukiongezeka kila mwaka. Vijana wengi kutoka Afrika wanatamani kuja kusoma hapa China hasa kutokana na maendeleo makubwa kiuchumi na kielimu yaliyopatikana katika nchi hii.

    Kuna tofauti kubwa sana kati ya China na nchi zingine zilizowekeza au kufanya biashara na nchi za Kiafrika. Kuna baadhi ya nchi zilizoendelea hazina utaratibu wa kutoa elimu kwa vijana wa Kiafrika, na hata wakifanya hivyo, nafasi zinakuwa chache sana.

    Kwa sasa naweza kusema China inaongoza kwa kufadhili elimu kwa vijana kutoka barani Afrika. Karibu kila mji wenye vyuo vikuu hapa China hawakosi wanafunzi toka barani Africa na wote wanafurahia Elimu wanayoipata hapa.

    Pamoja na misaada mbali mbali inayotolewa na China barani Afrika ikiwemo kuendeleza miundo mbinu na uwekezaji, kwa mwaka China inatumia mamilioni ya shilingi kufadhili elimu kwa vijana kutoka Afrika.

    Hakuna nchi hata moja barani Afrika ambayo haina raia wa China ambae anafanya shughuli huko hasa ya kimaendeleo, pia wametoa ajira kwa wazawa wa nchi hizo kupitia makampuni ambayo yamewekeza kwenye nchi hizo.

    Moja ya miji yenye idadi kubwa ya wanafunzi kutoa Afrika hapa China ni Wuhan ambao pia unajulikana kama Afrika ya China. Mji huo upo kati kati ya China. Kuna wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki na Magharibi, ambao wameunda umoja wao kama zilivyo nchi zao. Umoja huo unawasaidia sana katika kufanya mambo mbalimbali kuanzia kutatua matatizo ya binafsi hadi ya kimasomo. Jambo hili ni la kujivunia sana, na nchi nyingine zimepiga hatua zaidi maana hadi zina umoja wa wanafunzi wao wote wanaosoma hapa China.

    Baadhi ya nchi hizo ni kama Ghana, Nigeria, Uganda na huku wanafunzi kutoka Tanzania wakifanya harakati za kuanzisdha umoja kama huo. Kuna baadhi ya miji ambayo hakuna umoja wa wanafunzi kutokana na kuwa na wanafunzi wachache wa kigeni. Moja ya miji hiyo ni Nanchang ambao kwa sasa hakuna umoja wowote wa wanafunzi ila nimesikia kuna umoja wa wanafunzi kutoka Ghana ambao wapo wengi kwenye mjii huu kuliko wanafunzi toka nchi zingine za Afrika.

    Mwanafunzi mmoja kutoka nchini Ethiopia anasema China ina nia njema na ya kweli kwa bara la Afrika kuliko nchi nyingine duniani, maana kukubali kutoa elimu kwa vijana kutoka Africa ni swala la muhimu sana kwenye dunia ya sasa. Anasema ukiangalia jinsi vijana wengi wa Kiafrica wanaopata elimu hapa nchini China, unapata jibu kabisa kuwa China ina mpango wa kweli wa kuikomboa Afrika kielimu, na kwa hilo, anaipongeza sana China.

    Kweli kabisa China ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine kwa kuiokoa Africa kwenye swala la Elimu, ambalo ni swala muhimu sana kwa wakati huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako