Waswahili wanasema mambo mengi yana fanana hapa Duniani, kama halipo hapa basi lipo huko au kule, na hilo ndilo linalosemwa kwenye baadhi ya mambo ya jamii tofauti hapa duniani toka tabia moja hadi nyingine.
wakati wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka, Christmas na mwaka mpya, wachaga wengi nchini Tanzania, wanarejea makwao toka sehemu mbali mbali kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu hizo, na hilo limekuwa ni suala la kawaida sana na limeshazoeleka kwa Watanzania wengi, na usafiri wa kwenda mikoani huwa wa taabu sana.
Nchini China hivi sasa, wanakaribia kuadhimisha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, inayoitwa Chun jie , karibu wachina wote wamerejea maskani yao, kwa ajili ya kuadhimisha mwaka mpya huo.
Hivi sasa kila chombo cha usafiri kimejaa hapa China, kuanzia usafiri wao mkubwa wa Treni, Mabasi hata Ndege, hakuna nafasi.
Inakadiriwa zaidi ya wachina milioni 250, watasafiri ndani ya China kwa ajili ya kwenda nyumbani kwao kukutana na jamaa zao ili kusheherekea kwa pamoja mwaka mpya wa jadi wa China "Chun jie", kati ya hao milioni 37, watatoka Shanghai ambao ni mji wa kibiashara, milioni 21 watatoka mji mkuu Beijing.
kama ilivyo wachanga kule Tanzania, na wachina wakienda makwao wanapenda sana kula vyakula vyao vya asili, na kwa kipindi chote cha mwaka mzima wanakuwa mbali na familia zao hivyo wakati huu ni wakati wa kujumuika na familia, na kuelezana mawili matatu na kujipanga upya kwa maisha yajayo ya mwaka mwingine.
katika sherehe hizi cha mwaka mpya wa jadi wa China, shughuli zote zinafungwa kama mabenki, huduma za simu, kwa ujumla huduma zote muhimu zinafungwa isipokuwa hospitali, polisi, na vyombo vya habari kwa kuwa vinafanya kazi kwa zamu.
Zhou Qing wa hapa China anasema kwenye sikuku hii ni upweke mtupu kwa wageni kwa sababu marafiki zao wote wa China wanaondoka na kwenda makwao na ni lazima kurudi makwao kwa sababu wana desturi ya kufanya matambiko ya asili kwa ajili ya kuomba mema kwa maisha yao yajayo ya miezi mingine 12 ijayo.
Dada huyo anasema katika wakati wa sikukuu ya Chun jie ya mwaka jana alialikwa na rafiki yake wa Kichina kwenda kwao wakati wa sikuku hiyo na alikwenda kufanya matambiko ya asili ya Kichina, na kusema alipendezwa sana baada ya kuona wachina wanavyothamini mila na tamaduni zao.
Mbali na mila zifanywazo katika sherehe hizi pia miji yote inapendeza sana kwa mapambo ya rangi nyekundu na ya kimanjano. Sikukuu ya Chun jie, hiyo ndio sikukuu muhimu zaidi ya hapa China, maana sherehe inapendeza ukiwa nyumbani na familia yako.
mwisho kabisa nakutakia CHUN JIE KUAILE....yaani Happy Chun jie, furaha ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |