• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwogeleaji wa Afrika Kusini avunja rekodi ya Dunia na kujizolea medali ya dhahabu

    (GMT+08:00) 2012-07-30 11:09:07

    Kwenye uogeleaji mita 100 Breastroke kwa wanaume,muogeleaji Cameron van der Burgh wa Afrika Kusini aliivunja rekodi ya dunia na kujizolea medali ya dhahabu. Van der Burgh alivunja rekodi hiyo ya sekunde 58.98 iliyoandikishwa mwaka 2009 na kuandikisha muda mpya wa sekunde 58.46.

    China imeshinda medali ya kwanza ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki baada ya Yi Siling kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kulenga shabaha mita 10 kutumia bunduki kwa kina dada.Mnyanyuaji vyuma kitengo cha kilo 48 kwa kina dada. Mingjuan Wang Mingjuan wa China aliongeza idadi ya medali za dhahabu kwa nchi yake baada ya kuibuka na ushindi. Muogeleji Sun Yang alijinyakulia medali ya dhahabu kwenye mchezo wa uogeleaji mita 400 freestyle kwa wanaume nae Ye Shiwen pia ni mwogeleaji wa China alivunja rekodi ya Olimpiki na kushinda nishani ya dhahabu kwenye uogeleaji kitengo cha mita 400 medley kwa kina dada.

    Bado kwenye uogeleaji, Mmarekani Ryan Lochte amemshinda raia mwenza na bingwa mara mbili wa olimpiki, Michael Phelps na kunyakua nishani ya dhahabu kwenye kuogelea mita 400 medley.Aidha Phelps aliyetawala mchezo wa uogeleaji kwenye olimpiki mjini Athens,Ugiriki na Beijing,China aliibuka wa nne.Muogeleaji Thiago Pereira wa Brazil aalijinyakulia nishani ya fedha nae Kosuke Hagino wa Japan akitosheka na nishani ya shaba. Bado

    Kwenye soka kwa wanaume,Mabingwa wa dunia na bara Ulaya,Hispania wameiaga olimpiki baada ya kufungwa goli moja bila jawabu na Honduras kwenye hatua ya kimakundi ya kundi D.Aidha mechi nyingine ya kundi hilo ilishuhudia Japan ikisongea mbele baada ya kupata ushindi finyu wa goli moja kwa sufuri dhidi ya Morocco.Kwenye kundi C,Brazil iliichapa Belarus magoli matatu kwa moja huku Misri ikitoka sare ya goli moja na New Zealand.Mechi ya kundi B ilishuhudia Mexico ikiiadhibu Gabon magoli mawili bila jawabu nayo Korea Kusini ikapata ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Uswizi.

    Timu ya wanaume ya Italia imeishinda Marekani kwa pointi moja hivyo kujizolea nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa kulenga kwa mshale kwa timu.Aidha Marekani ilijipatia nishani ya fedha huku Korea Kusini ikitosheka na medali ya shaba baada ya kuishinda Mexico.Kwenye mchezo wa mpira wa vikapu kw kina dada,Australia ilianza vyema kwa kuishinda Uingereza kwa pointi 78 dhidi ya 58.Mabingwa wa Olimpiki,Marekani waliishinda Croatia kwa pointi 81 kwa 56,Russia ikapata pointi finyu za 58 kwa 53 dhidi Canada nayo Ufaransa ikaifunza adabu Brazil kwa pointi 73 kwa 58.Mabingwa wa Afrika,Angola ambao wanashiriki olimpiki kwa mara ya kwanza walipewa kichapo cha pointi 72 kwa 50 na Uturuki huku China ikijizatiti kupata pointi 66 kwa 57 za Jamuhuri ya Czech.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako