• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Kenya ya wanariadha 30 wa ndani na nje chaelekea jijini London

    (GMT+08:00) 2012-07-31 10:33:07

    Timu ya Kenya ya wanariadha 30 wa ndani na nje kimeelekea jijini London na kuahidi kufanya vyema kuliko olimpiki ya Beijing.Timu hiyo ya Kenya chini ya uongozi wa bingwa wa dunia wa mbio za mita 800,David Rudisha,ni mojawapo wa zilizofika kuchelewa kwenye mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi ijumaa iliyopita.Kando na mbio za mita 800,Rudisha pia atashiriki mbio za mita 400 za kupokezana vijitiMwanariadha Vivian Cheruiyot pia atashiriki mbio za mita 5000 na 10000 kwa kina dada.Maneja wa timu hiyo,Joesph Kinyua amesema wanariadha sita wa mbio za mita 5000 na wa mbio za masafa marefu watabakia Nairobi,Kenya na kujiunga na wenzao Agosti 7.Ratiba ya riadha inatarajiwa kuanza Agosti 3.

    Kaori Matsumoto wa Japan amejizolea nishani ya dhahabu kwenye judo upande wa kina dada wa uzani wa kilo 57 baada ya kumshinda mpinzani wake, Corina Caprioriu wa Romania.Marti Malloy wa marekani na Automne Pavia wa Ufaransa kila mmoja akajizolea nishani ya shaba.Bado kwenye judo ya kina dada uzani wa kilo 52, Kum Ae An aliipatia Korea Kaskazini nishani yake ya kwanza ya dhahabu baada ya kumshinda Yanet Bermoy Acosta wa Cuba.

    Muogeleaji Yannick Agnel wa Ufaransa alichapa maji kwenye mchezo huo mita 200 freestyle na kujizolea medali ya dhahabu.Aidha Sun Yang wa China na Park Tae Hwan wa Korea Kusini wakajizolea nishani za fedha baada ya kuandikisha muda sawa.Timu ya China ya mchezo wa upigaji mbizi ilishinda medali zote nane za dhahabu baada ya Cao Yuan na Zhang Yanquan kushinda mbizi mita 10 upande wa wanaume.wakati huohuo, Ye Shiwen wa China aliregea kidimbwini tena kushiriki mchujo katika uogeleaji mita 200 medley ambapo aliibuka na ushindi baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya mita 400 medley kwa kina dada. Federica Pellegrini wa Italia alifuzu wa kwanza kwenye kuogelea mita 200 freestyle.Kwenye kuogelea upande wa wanaume mita 200 butterfly, Dinko Jukic wa Austria aliweza kufuzu wa kwanza.

    Timu ya China ya wanaume ya mchezo wa artistic gymnastics ilijipindapinda nakupata pointi nne zaidi hivyo kujinyakulia nishani ya dhahabu nakuilazimisha Japan kuridhika na nishani ya fedha.Aidha wenyeji wa olimpiki,Uingereza walitosheka na medali ya shaba.Hii ilikuwa medali ya kwanza kwa Uingereza kushinda kwenye olimpiki tangu michezo ya mwaka 1912 mjini Stockholm,Sweden.wakati huohuo mnyanyuaji vyuma wa China,Li Xueying aliandikisha rekodi mpya za olimpiki na kushinda medali ya dhahabu kwenye kitengo cha kina dada cha kilo 58.

    Kwenye Mchezo wa mpira wa vinyoya kwa kina dada,wachezaji Wang Yihan na Wang Xin wa China walifika hatua ya 16 bora kwa urahisi baada ya kuwashinda Michele Li wa Canada na Wang Rena wa Marekani mtawalia.kwa upande wa wanaume, Niluka Karunaratne wa Sri Lanka alimshinda Kenichi Tago wa Japan.kwenye mchezo huo kwa upande wa wachezaji wawili, Tian Qing na Zhao Yunlei wa China waliwaondoa Miyuki Maeda na Satoko Suetsuna wa Japan nao Joachim Fischer na Christinna Pedersen wa Denmark wakapata ushindi dhidi ya Robert Mateusiak na Nadiezda Zieba wa Poland.

    Kwenye mpira wa mkono kwa kina dada,Korea Kusini iliishinda Denmark kwa magoli 25 kwa 24 na kujikatia tiketi ya robo fainali.

    Tuangazie mpira wa magongo kwa wanaume ambapo Australia iliendeleza mchakato wake wa kutafuta nishani ya dhahabu kwa kuichakaza Afrika Kusini magoli sita bila jawabu.

    Mpira wa vikapu kwa kina dada…China iliendelea na msururu wake wa ushindi kwa kuifunga Croatia vikapu 83 dhidi ya 58. Wawakilishi wa bara Afrika,Angola waliendelea kuandikisha matokeo ya kuvunja moyo huku ikishikilia mkia kwenye kundi lake.Aidha kwenye mchezo wa voliboli kwa kina dada China iliishinda Uturuki kwa seti tatu kwa moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako