• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya nane ya mashindano ya olimpiki tuangazie yalojiri viwanjani

    (GMT+08:00) 2012-08-05 19:26:06

    Tuanze na riadha,kwenye mbio za mita 10000 kwa wanaume, Mo Farah wa Uingereza alijishindia nishani ya dhahabu, Galen Rupp wa Marekani akajibebea nishani ya fedha nae Bekele Tariku wa Ethiopia akavuna medali ya shaba.Mbio za mita 100 kwa kina dada zilishuhudia Shelly-Ann Fraser-Pryce na Veronica Campbell-Brown wa Jamaica wakijipatia nishani za dhahabu na shaba mtawalia.Aidha Carmelita Jeter wa Marekani akaridhika na nishani ya fedha.

    Kwenye mchezo wa kuogelea,kuendesha baiskeli na kukimbia yaani Triathlon kwa kina dada, Spirig Nicola wa Uswizi alijinyakulia nishani ya dhahabu, Norden Lisa wa Sweden akajitwita medali ya fedha nae Erin Densham wa Australia akaridhika na nishani ya shaba.

    Mchezo wa kupiga makasia wa mtu mmoja kwa kina dada ulishuhudia Knapkova Miroslava wa Jamuhuri ya Czech akijitwalia nishani ya dhahabu, Erichsen Fie Udby wa Denmark akajipatia medali ya fedha nae Crow Kim wa Australia akatosheka na nishani ya shaba.bado kwenye mchezo huo kwa kutumia makasia mawili kwa timu ya watu wawili kwa kina dada,Copeland Katherine na Hosking Sophie wa Uingereza walijipatia nishani ya dhahabu, Xu Dongxiang na Huang Wenyi wa China wakapokea medali ya fedha nao Giazitzidou Christina na Tsiavou Alexandra wa Ugiriki wakatosheka na nishani ya shaba.kwa upande wa wanaume, Rasmussen Mads na Quist Rasmus wa Denmark waliibuka na medali ya dhahabu, Purchase Zac na Hunter Mark wakajaza kikapu cha Uingereza kwa medali ya fedha nao Uru Storm na Taylor Peter wakajipatia nishani ya shaba.Bado kwenye mchezo huo kwa timu ya watu wanne kwa wanaume,timu ya Uingereza ilijipatia nishani ya dhahabu,Australia wakajinyakulia nishani ya fedha nayo Marekani ikatia mkobani medali ya shaba.

    Jamie (Beyerle) Gray wa Marekani alijinyakulia medali ya dhahabu kwenye mchezo wa kulenga shabaha mita 50 kutumia bunduki kwa kina dada, Maksimovic Ivana wa Serbia akajibebea medali ya fedha nae Sykorova Adela wa Jamuhuri ya Czech akatosheka na nishani ya shaba.

    Serena Williams wa Marekani alijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa tenisi wa mtu mmoja kwa kina dada na kumlazimisha Maria Sharapova wa Russia kuchukua medali ya fedha.Aidha Victoria Azarenka wa Belarus na KirilenkoMaria wa Russia wakangangania nishani ya shaba.Kwa upande wa wanaume wa timu ya watu wawili,Mike na Bob Bryan wa Marekani walinyakua medali ya dhahabu.

    Kwenye mchezo wa uwindaji kutumia bunduki aina ya shotgun yaani TRAP wa mtu mmoja kwa kina dada, Rossi Jessica wa Italia alifanikiwa kujipatia nishani ya dhahabu, Stefecekova Zuzana wa Slovakia akajitwalia medali ya fedha nae Reau Delphine wa Ufaransa akajitwika medali ya shaba.

    Mbele ya mashabiki 80000, mwanamichezo Jessica Ennis wa Uingereza alishinda nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa Heptathlon.Ennis alijizolea pointi 6995,pointi za juu za tatu kwenye historia ya mashindano ya olimpiki

    Siku kadha baada ya wachezaji wake wawili kupigwa marufuku,timu ya kina dada ya watu wa wawili ya mpira wa vinyoya ya Tian Qing na Zhao Yunlei wa China ilijipatia nishani ya dhahabu,Fujii Mizuki na Kakiiwa Reika wa Japan wakajitilia mkobani nishani ya fedha nao Sorokina Valeria na Vislova Nina wa Russia na Bruce Alex na Li Michele wa Canada wakagawana medali ya shaba.Aidha Li Xuerui wa China alijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye kitengo cha mchezaji mmoja.

    Tuangazie sasa mchezo wa turubali yaani Trampoline kwa kina dada, Rosie MacLennan wa Canada alichukua medali ya dhahabu,Huang Shanshan na He Wenna wa China wakajitwalia nishani za fedha na shaba mtawalia.

    China iliendeza msururu wa kujinyakulia medali kwenye mchezo wa kutembea kwa kasi kilomita 20 kwa wanaume huku Chen Ding na Wang Zhen wakijitwika medali za dhahabu na shaba mtawalia. Barrondo Erick wa Guatemala akajipatia nishani ya fedha.Aidha Ding mwenye umri wa miaka 19 amekuwa mchina wa kwanza kushinda nishani ya dhahabu kwenye mchezo huo

    Timu ya Uingereza ya Uingereza ya watu wawili kwa wanaume ya Uendeshaji baiskeli ilijinyakulia nishani ya dhahabu,Marekani ikajitwalia medali ya fedha nayo ile ya Canada ikavuna medali ya shaba.

    Tujitose kidimbwini ambapo mwanadada Kromowidjojo Ranomi wa Uholanzi aliibuka na medali ya dhahabu kwenye uogeleaji mita 50 freestyle kwa kina dada huku raia mwenza, Veldhuis Marleen akiridhika na nishani ya shaba. Herasimenia Aliaksandra wa Belarus akavikwa medali ya fedha.kwa upande wa wanaume wa mita 1500 freestyle, Sun Yang wa China aliibuka na medali ya dhahabu na kuivunja rekodi yake ya dunia, Cochrane Ryan wa Canada akajipatia medali ya fedha nae Mellouli Oussama wa Tunisia akaridhika na nishani ya shaba.Bado tusalie kidimbwini ambapo timu ya kina dada ya Marekani ilijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye uogeleaji wa nne kwa mita 400 medley kupokezana,timu ya Australia ikabeba nishani ya fedha nayo ile ya Japan ikajipatia medali ya shaba.Kwa upande wa wanaume,Timu ya Marekani chini ya uongozi wa Michael Phelps ilijitwika nishani ya dhahabu.Aidha timu ya Japan na ile ya Australia zikatosheka na nishani za fedha na shaba mtawalia.Phelps ametangaza kustaafu punde baada ya olimpiki kukamilika.

    Kwenye mchezo wa kutupa kisahani kwa kina dada, Sandra Perković wa Croatia alijitwalia medali ya dhahabu, Pischalnikova Darya wa Russia akajipatia medali ya fedha nae Li Yanfeng wa China akaikumbatia nishani ya shaba.

    Rutherford Greg wa Uingereza aliipa fahari nchi yake kwa kujizolea nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa Long Jump kwa wanaume.Aidha Watt Mitchell wa Australia na Will Claye wa Marekani wakaridhika na nishani za fedha na shaba mtawalia.

    Tuangalie meza ya medali kufikia sasa…..

    JUMLA Dhahabu Fedha Shaba

    1. Marekani 54 26 13 15

    2. China 54 25 16 13

    3. Uingereza 29 14 7 8

    4. Korea Kusini 18 9 3 6

    5. Ufaransa 22 8 6 8

    12. Afrika Kusini 4 3 1 0

    28. Ethiopia 2 1 0 1

    40. Kenya 2 0 1 1

    46. Misri 1 0 1 0

    52. Tunisia 1 0 0 1

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako