• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya 10 ya mashindano ya Olimpiki jijini London,Uingereza. Tuangazie matokeo ya michezo mbalimbali.

    (GMT+08:00) 2012-08-06 10:32:40

    Tuanze na riadha ambapo kwenye mbio za mita 3000 kuruka viunzi,Ezekiel Kemboi wa Kenya aliipatia nchi yake medali ya kwanza ya dhahabu huku raia mwenza Abel Kiprop Mutai akichukua medali ya shaba.Mahiedine Mekhissi-Benabbad wa Ufaransa alivikwa medali ya fedha.

    Kwenye mbio za marathon kwa wanawake, Gelana Tiki wa Ethiopia alijivunia nishani ya dhahabu, Jeptoo Priscah wa Kenya akajichukulia nishani ya fedha nae Petrova Arkhipova Tatyana wa Russia akatosheka na medali ya shaba.

    Wakati huohuo mwanariadha Usain Bolt wa Jamaica alidhihirisha ubabe wake kwenye mbio za mita 100 kwa wanaume kwa kuchukua nishani ya dhahabu.Bolt mwenye umri wa miaka 25 amekuwa mwanariadha wa pili kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya olimpiki kwa kufuatana.Mwanariadha Carl Lewis wa Marekani alifanikisha hilo kwenye olimpiki mwaka 1984 na 1988.Aidha Yohan Blake wa Jamaica alijitwalia medali ya fedha nae Justin Gatlin wa Marekani akatosheka na nishani ya shaba.

    Wakati hayo yakiarifiwa,Mwanariadha Oscar Pistorius wa Afrika Kusini alishindwa kufuzu kwenye mbio za mita 400 kwa wanaume hivyo kuzima ndoto yake ya olimpiki. Pistorius aliweka historia jumamosi kwa kuwa mtu wa kwanza kushiriki olimpiki akiwa na miguu bandia kutokana na miguu yake kukatwa chini ya magoti akiwa mtoto.Aidha Pistorius ataregea tena kushiriki mbio za mita 400 kupokezana vijiti kwa wanaume na pia atashiriki olimpiki ya walemavu.

    Kina dada ndugu wa Marekani,Vanessa na Serena Williams walijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa tenisi wa timu ya watu wawili kwa kina dada.HlavackovacAndrea na Hradecka Lucie wa Russia wakajitwalia nishani ya fedha.

    Jin Jongoh na Choi Young Rae wa Korea Kusini walitawala mchezo wa kulenga shabaha kutumia bastola mita 50 kwa wanaume kwa kujizolea nishani ya dhahabu na fedha mtawalia.Wang Zhiwei wa China akajibebea medali ya shaba.

    Mchezo wa Gymnastics zoezi la sakafuni kwa wanaume ulishuhudia Zou Kai wa China akijishindia medali ya dhahabu, Kohei Uchimura wa Japan akatosheka na medali ya fedha nae Ablyazin Denis wa Russia akavikwa nishani ya shaba.kwenye mchezo huo upande wa kina dada kutumia upondo, Sandra Izbasa wa Romania alichukua nishani ya dhahabu, McKayla Maroney wa Marekani akajitwalia nishani ya fedha nae Paseka Maria wa Russia akavikwa nishani ya shaba.Tusalie kwenye mchezo huo kwa upande wa wanaume Pommel Horse, Berki Krisztian wa Hungary alijishindia nishani ya dhahabu, Louis Smith na Whitlock Max wa Uingereza wakaridhika na nishani za fedha na shaba mtawalia.

    Lin Dan wa China alijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa mpira wa vinyoya wa mtu mmoja kwa wanaume. Lee Chong Wei wa Malaysia akajipatia medali ya fedha.Chen Long pia wa China alijivunia medali ya shaba.Kwa upande wa timu ya watu wawili ya wanaume, Cai Yun na Fu Haifeng wa China walijitwika nishani ya dhahabu,Boe Mathias na Mogensen Carsten wa Denmark wakatosheka na medali ya fedha nao Chung Jae Sung na Lee Yong Dae wa Korea Kusini wakachukua medali ya shaba.

    Andy Murray wa Uingereza aliweza kuinua hadhi ya nchi yake kwa kujizolea nishani ya dhahabu na kumlazimisha Roger Federer wa Uswizi kujitwalia nishani ya fedha kwenye mmchezo wa tenisi wa mtu mmmoja kwa wanaume. Delpotro Juan Martin wa Argentina akajichukulia medali ya Shaba.

    Mwanadada Zhou Lulu wa China alinyanyua nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa unyanyuaji vyuma kwa kina dada kitengo cha kilo 75, Kashirina Tatiana wa Russia akajivunia nishani ya fedha nae Khurshudyan Hripsime wa Armenia akajipatia nishani ya shaba.

    Mchezo wa kupiga mbizi kwa wanawake mita tatu ulishuhudia kina dada Wu Minxia na He Zi wa China wakijitwalia nishani za dhahabu na fedha mtawalia na kumwachia nishani ya shaba Laura Sanchez wa Mexico.

    Tuangazie mchezo wa masumbwi kwa kina dada hatua ya robo fainali uzani wa kilo 75 ambapo Elizabeth Andiego wa Kenya alishindwa kustahimili makonde ya Marina Volnova wa Kazakhstan,Li Jinzi wa China akamchubua sura Roseli Feitosa wa Brazil nae Edith Ogoke wa Nigeria akampapura Elena Vystropova wa Azerbaijan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako