• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ni ya 13 kwenye mashindano ya olimpiki jijini London,Uingereza.

    (GMT+08:00) 2012-08-09 10:28:31

    Aliyekuwa bingwa wa mbio za Marathon kwa wanaume, Douglas Wakiihuri wa Kenya ameupa changamoto uteuzi wa timu ya mbio za mita 10,000 wa nchi hiyo kwenye mashindano ya olimpiki. Wakiihuri ameongeza kuwa timu hiyo ilikuwa ipate matokeo mabaya kutokana na na njia iliyotumika kuiteua. Mwanariadha huyo mstaafu ambaye alishinda medali ya fedha kwenye olimpiki mwaka 1988 mjini Seoul, Korea Kusini amedokeza kuwa ingewachukua kazi kubwa wanariadha Moses Masai, Wilson Kiprop na Bedan Karoki ambao wanashiriki mbio za barabarani kumshindwa Mo Farah wa Uingereza. Aidha Wakiihuri ameongeza kuwa kuna tofauti kubwa ya mbio za barabarani na zile za uwanjani huku akidadisi hekma ya chama cha riadha Kenya(AK) kuhusu kufanyia timu hiyo majaribio mjini Oregon,Marekani. Wakiihuri ambaye pia alishinda taji la dunia la Marathon mwaka 1987 amewalaumu maafisa wa AK na kusema wanariadha wa Kenya wamekuwa wakishinda medali wakifanya mazoezi nyumbani na sio nje ya nchi. Mara ya mwisho kwa Kenya kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 kwa wanaume ilikuwa mwaka 1968 ambapo mwanariadha Naftali Temu aliibuka na ushindi. Aidha mwanariadha Paul Tergat alishinda medali ya fedha kwenye olimpiki ya Atlanta, Marekani mwaka 1996 na Sydney, Australia mwaka 2000. Kwenye olimpiki jijini Beijing,China Mwanariadha Micah Kogo aliishindia nchi hiyo medali ya shaba.

    Bado kwenye riadha,Aries Merritt wa Marekani aliandikisha muda binafsi bora na kujinyakulia medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 110 kuruka viunzi kwa wanaume,Ni medali ya kwanza ya dhahabu kwa Marekani kushinda tangu olimpiki ya mjini Atlanta mwaka 1996 ambapo mwanariadha Allen Johnson aliibuka na ushindi.Jason Richardson pia wa Marekani alijitwalia medali ya fedha nae Hansle Parchment wa Jamaica akavuna nishani ya shaba.kwenye mbio za mita 200 kwa kina dada,Allyson Felix na Carmelita Jeter wa Marekani walibeba nishani za dhahabu na shaba mtawalia na kumlazimisha Shelly Ann Frazier-Pryce wa Jamaica kujiliwaza na medali ya shaba.Mbio za mita 400 kwa kina dada zilishuhudia Natalya Antyukh wa Russia akijitwalia nishani ya dhahabu.Aidha mwanadada Britney Reese wa Marekani alivikwa nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa long jump kwa kina dada

    Kwenye mchezo wa mpira wa wavu wa ufukweni(Beach Volleyball) kwa timu ya watu wawili kwa kina dada,Misty May-Treanor na Kerri Walsh wa Marekani walivikwa medali ya dhahabu.

    Mwanadada Wu Jingyu wa China aliweza kukumbatia medali ya dhahabu kwenye mchezo wa taekwondo kitengo cha kilo 49 baada ya kumpa kipigo cha kutosha bingwa mara tatu wa dunia Brigitte Yague wa Hispania.Kwa upande wa wanaume kitengo cha kilo 58,Joel Gonzalez wa Hispani aliipatia nchi yake medali ya kwanza ya dhahabu kwenye mchezo huo baada ya kumtwanga Lee Dae Hoon wa Korea Kusini.

    Larsen Eirik Veras wa Norway alijizolea nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa Kayaki kwa wanaume kitengo cha K-1 mita 1000, van Koeverden Adam wa Canada akavikwa medali ya fedha nae Hoff Max wa Ujerumani akajitwalia nishani ya shaba.Bado kwenye mchezo huo kitengo cha C-1 mita 1000, Brendel Sebastian wa Ujerumani aliibuka na medali ya dhahabu, Cal Figueroa David wa Hispania akakumbatia nishani ya fedha nae Oldershaw Mark wa Canada akatosheka na medali ya shaba.Kwenye mchezo huo wa timu ya watu wawili kwa wanaume, Dombi Rudolf na Kokeny Roland wa Hungary walijibebea nishani ya dhahabu, Pimenta Fernando na Silva Emanuel wa Ureno wakajizolea nishani ya fedha nao Hollstein Martin na Ihle Andreas wa Ujerumani wakaridhika na nishani ya shaba.kwa upande wa kina dada kwa timu ya watu wanne mita 500,timu ya Hungary iliibuka na medali ya dhahabu,Ujerumani wakajitwika medali ya fedha nayo ile ya Belarus ikakumbatia nishani ya shaba

    Mchezo wa kuendesha mashua kwa timu ya watu wawili 49er kwa wanaume, Nathan Outteridge na Iain Jensen wa Australia walinyanyua nishani ya dhahabu, Peter Burling na Blair Tuke wa New Zealand wakavikwa medali ya fedha nao Allan Norregaard na Peter Lang wakatia mkobani nishani ya shaba.

    Guerdat Steve wa Uswizi alijinyakulia nishani ya dhahabu kwenye mchezo wa ujuzi wa kumpeleka farasi kwa wanaume, Schroder Gerco wa Uholanzi akaikumbatia medali ya fedha nae O'Connor Cian wa Ireland akavuna nishani ya shaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako