• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bara la Afrika kuwakilishwa na timu 5 kwenye kombe la Dunia

    (GMT+08:00) 2014-04-23 10:59:42

    Bara la Afrika safari hii litawakilishwa na timu 5 kwenye kombe la Dunia huko Brazil. Timu hizo ni pamoja na Aljeria, Nigeria, Ghana, Ivory Coast na Cameroon. Timu ya taifa ya Cameroon almaarufu kama "The Indomitable Lions" ni miongoni mwa nchi zilizofuzu kucheza kombe la dunia mwaka huu huko Brazil, na imeshiriki mara 6 kwenye kombe hilo, haijawahi kushinda taji hili, pia iko katika nafasi ya 50 kwenye viwango vya FIFA. Katika michuano ya kufuzu ilikuwa kundi moja na Libya, DRC na Togo. Cameroon ilimaliza michuano ya mataifa ya Afrika ikiwa na pointi 13 kutokana na mechi 6. Katika raundi ya mwisho ya mchujo walikuwa na kibarua kigumu dhidi ya Tunisia. Sare ya tasa iliwapa njia ya kuelekea Brazil baada ya mechi ya nyumbani waliyoshinda 4-1dhidi ya Tunisia.

    Licha ya kuwa hakuna timu toka barani Afrika ambayo imewahi kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia la FIFA, timu ya taifa ya Cameroon itakumbukwa kwa yale iliyoyafanya kwenye fainali za mwaka 1982 zilizofanyika nchini Hispania na kumaliza bila kufungwa kwenye hatua ya makundi. Katika mashindano hayo Cameroon ilitoka sare ya bila kufungana na timu ya Peru, huku dhidi ya Poland wakiishia 1-1 ambapo mwaka huo Italy ilichukua ubingwa.

    Miaka minane baadaye waliingia kwenye kumbukumbu baada ya kuwashinda mabingwa watetezi Argentina katika mechi ya ufunguzi na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali, baada ya magoli yaliyofungwa na mshambuliajii wa evergreen wa wakati huo Roja Milla.

    Cameroon Cameroon sio timu ya kuipuuza hata kidogo katika fainali za mwaka huu za Brazil. Cameroon ambayo imekuwa katika kiwango bora cha FIFA kwa Afrika, lakini pia imeshiriki fainali hizo mara nyingi zaidi kuliko taifa jingine la Afrika. Pia hakuna timu ya Afrika iliyowahi kufikia rekodi yake ya kufika robo fainali mwaka 1990, hadi Senegal ilipofikia rekodi hiyo mwaka 2002. Cameroon haijawahi kuvuka hatua ya makundi katika fainali tatu ilizoshiriki ikishinda mechi moja tu kati ya tisa ilizocheza. Timu hii pia imeshiriki kwenye michuano ya mwaka 1994, 1998, 2002 na 2010

    Kwa upande wa wachezaji wake wakubwa, Samuel Eto'o bado anabaki kuwa tishio kubwa kwa timu nyingine, na ingawa mchezaji wake mwenye ushawishi ambaye anacheza kama kepteni wa timu hiyo, kuwa akitoka na kurejea kwenye timu, lakini hata bila kuwepo veterani wa Chelsea, timu hiyo ikiwa na wachezaji wenye kipaji na uzoefu mkubwa kama vile Nicolas N'Koulou, Benoit Assou-Ekotto na Aurelien Chedjou bado ni ina nguvu katika ulinzi, huku ikiwa imejaza viungo viungo wa kati kama vile Alex Song, Jean Makoun and Stephane Mbia.

    Cameroon Haikushiriki fainali za 2006 nchini Ujerumani lakini kufuzu kwa fainali hizi za Brazil Wacameroon wengi wanaamini kuwa ni kuwepo kwa mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na wachanga ambao sasa wanatoa damu itakayorithi kizazi cha akina Roger Millas na Francois Omam-Biyiks.

    Cameroon iliondolewa katika hatua ya makundi nchini Hispania mwaka 1982 na imecheza mechi kumi na nane zinazoandaliwa na FIFA ikiwa ni zaidi ya taifa lolote la Afrika. Roger Milla aliandika rekodi ya kuwa mchezaji aliyeshiriki fainali za kombe la dunia akiwa na umri wa miaka 42 na siku 39 alipofunga bao dhidi ya Russia katika fainali za mwaka 1994.

    Cameroon ikiwa chini ya Kocha Volker Finke safari hii ipo kwenye kundi A pamoja na wenyeji wa michuano hii Brazil, Croatia na Mexico. Mechi yake ya kwanza itakuwa tarehe 13 Jun ambapo watakwaana na Mexico saa saba mchana kwa saa huko katika uwanja wa Estadio das Dunas. Katika michuano ya mwaka 2010 nchini Afrika Kusini Cameroon waligaragazwa na Japan kwa 1-0 katika hatua ya makundi, ambapo kwa siku hiyo machachari yao hayakuonekana sana, kwani Japan ilionekana kuumiliki mpira na kucheza kitimu yaani kwa ushirikiano mkubwa. Kwa hiyo tusubiri katika mechi yake ya mwanzo dhidi ya Mexico Eto'o ataonesha machachari yake na ufundi wake tutajua siku hiyo ya tarehe 13 Juni.

    (pili)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako