Mchezaji wa klabu ya Ac Bongoville, Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke la kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon. Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitali baada ya tokeo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelisimamisha kombora lililopigwa langoni mwake, lakini mshambuliaji alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani. Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa huko Bongoville umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |