• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu za Afrika zinazoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil

    (GMT+08:00) 2014-04-29 11:25:56

    Wiki iliyopita tuliizungumzia timu ya taifa ya Cameroon ambayo maarufu inajulikana kama "The Indomitable Lions", tulisema kuwa ni timu pekee iliyoitoa kimasomaso Afrika na kufika kwenye hatua ya fainali katika kombe la dunia. Pia kwa mara ya kwanza iliingia katika kombe la dunia mwaka 1982. Lakini leo hii tutaigeukia Côte d'Ivoire ama "Tembo wa Afrika" ambayo nayo pia ni miongoni mwa nchi 5 za Afrika zilizofuzu kucheza kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil. Ila kabla ya kukuelezea kwa undani kuhusu timu hii kwanza tusikilize kibao hicho

    Kama tulivyosema awali Afrika inawakilishwa na nchi 5 katika kombe la dunia la Brazil linalotarajiwa kutimua vumbi Juni 12. Miongoni mwa nchi hizo tano Côte d'Ivoire nayo pia imo ndani. Côte d'Ivoire Imeshiriki mara 2 katika kombe la dunia ambapo pamoja na mwaka huu itakuwa ni mara ya tatu kushiriki kwenye kombe hilo. Mara ya kwanza kabisa ilianza kucheza kombe la dunia mwaka 2006, katika mwaka huo timu hiyo ilisaidia kufikiwa kwa makubaliano ya muda ya amani kati ya pande mbili zilizokuwa zikipambana nchini humo kwa kumshawishi rais Laurent Gbabo kuanza mazungumzo ya amani.

    Katika michuano ya kufuzu ya kombe la mataifa ya Afrika Côte d'Ivoire ilijipatia ushindi mara nne kati ya mechi 6 ilizocheza kwenye hatua ya makundi katika hatua ya robo fainali ilipocheza na Senegal walitoka sare ya 3-3 na kujihakikishia nafasi yao katika kombe la dunia kwa mara ya tatu. Côte d'Ivoire haijawahi kuvuka hatua ya makundi kwenye fainali za kombe la dunia, mara zote iliposhiriki haijafanya vizuri, na hii labda ni kutokana na makundi ambayo imekuwa ikipangiwa yaani kundi la kifo. Kwani Mwaka 2006 kwenye fainali zilizochezwa nchini Ujerumani, Côte d'Ivoire ilipangwa katika mkundi C na nchi kama Argentina, Uholanzi, Serbia na Montenegro na kumaliza kwenye nafasi ya tatu, baada ya kushindwa na Argentina na Uholanzi, lakini iliweza kuishinda Serbia na Montenegro na kupelekea kuishia hatua ya makundi. Ni sawa na walivyofanya miaka mine baadaye kwenye fainali za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini ambapo walipangiwa timu za Brazil, Ureno na Jamhuri ya Korea na pia kuishia hatua ya makundi.

    Safari hii Côte d'Ivoire ipo kwenye kundi C ikiwa pamoja na nchi kama vile Colombia, Ugiriki na Japan. Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa bado kundi hili ni gumu kwa timu ya Côte d'Ivoire na huenda kwa mara nyingine wakaishia kwenye hatua ya makundi. Côte d'Ivoire inajivunia kwa kuwa na wachezaji wakubwa wenye vipaji katika Afrika, na ni moja kati ya timu zilizosheheni wachezaji wanaocheza soka ya kulipwa Ulaya, mfano ni washambuliaji wake kama Didier Drogba na Solomon Kalou ambao wanaunda muungano mzuri mbele, wakati viungo kama Didier Zakora na Yaya Toure ni wachezaji muhimu viuongo wa timu hii, washambuliaji wa pembeni kama Gervinho na mabeki kama Emmanuel Eboue na kolo Toure pia ni miongoni mwa wachezaji tegemezi kwenye timu hii.

    Kama tulivyosema wiki iliyopita kuwa Rojamila alivuma sana kwenye timu ya taifa ya Cameroon kwa hiyo na Côte d'Ivoire pia inao wachezaji kama hao wakiwemo Laurent Pokou, Youssouf Fofana, na Joel Tiehi.

    Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire Tembo wa Afrika imejipatia mafanikio baada ya kushiriki fainali za kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, na zile za Afrika Kusini mwaka 2010 na kuondolewa kwenye hatua ya makundi, pia ilishiriki kwenye Kombe la dunia kwa vijana walio na umri wa chini ya miaka 17 nchini Canada mwaka 1987 na kumaliza kwenye nafasi ya tatu, na pia walicheza kombe la shirikisho la FIFA nchini Saudi Arabia mwaka 1992 na kumaliza kwenye nafasi ya nne.

    Hivi karibuni FIFA imeiweka Côte d'Ivoire nafasi ya kwanza katika viwango vyake kwa nchi za Afrika na kwa ujumla ipo kwenye nafasi ya 21 kwenye viwango vya FIFA. Katika mwaka 2006 Côte d'Ivoire ilikuwa ni nchi pekee kutaja kikosi chake cha wachezaji 23 wa kumbo la dunia ambacho kinaundwa na wachezaji ambao wanachezea klabi za soka nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako