• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la dunia Fifa Brazil World Cup 2014

    (GMT+08:00) 2014-05-06 10:59:50

    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zitakazocheza kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, tuliizungumzia Ivory Coast ama "Tembo wa Afrika" jinsi ilivyoweza kufuzu michezo ya safari hii na jinsi ilivyofanya katika michezo ya dunia kule nchini Ujerumani na Afrika Kusini. Pia tulisema kuwa ni timu ambayo haijavuka hatua ya makundi katika safari zake zote mbili ilizoshiriki michuano hii mikubwa na mafanikio mbalimbali iliyopata katika michuano mbalimbali duniani. Sasa katika kipindi cha leo tutaizungumzia timu ya taifa ya Nigeria na kuona jinsi ilivyofanya katika michuano iliyopita ya kombe la dunia lakini kabla ya kuendelea mbele tupate kitu hicho kutoka

    Kama tulivyosema awali kwamba leo hii ndani ya studio tutajadili timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama the Eagles. Katika michuano ya mabingwa wa Afrika ya kufuzu kombe la dunia timu hii ilikuwa katika kundi F pamoja na Malawi, Kenya na Namibia. Nigeria ilikuwa ikitumainiwa zaidi kufika raundi ya mtoano ya kuweza kufuzu, ambapo walifanya vizuri sana kwani hawakushindwa mechi hata moja katika hatua ya makundi, isipokuwa walitoka sare mara tatu, kwa kila mpinzani wake. Hata hivyo walipocheza na Kenya katika uwanja wao pia walitoka sare lakini wasiwasi ulitawala kwani Nigeria waliweza kusawazisha matokeo katika kipindi cha pili dakika za majeruhi wakati Nnamdi Oduamadi alipoingiza bao na kupelekea sare ya 1-1.

    Nigeria kwa mara ya kwanza ilianza kushiriki kombe la dunia mwaka 1994. katika mwaka huo iliwekwa katika kundi pamoja na Argentina, Bulgaria na Ugiriki. Katika mechi yake ya kwanza iliishinda Bulgaria kwa 3-0, baadaye ikashindwa na Argentina kwa 1-2 na hatimaye ikafuzu kucheza raundi ya pili baada ya kuilaza Ugiriki kwa magoli 2-0. katika raundi ya pili Nigeria ilicheza na Italy na kupata kuongoza baada ya Amunike kuingiza goli katika dakika ya 25. Ziliposalia dakika mbili mpira kuisha na Nigeria kuweza kufika hatua ya robo fainali, Italy ikaingiza goli na kupelekea mchezo kuongezwa muda, na hadi mechi inamalizika Italy walikuwa wanaongoza kwa 2-1. Mwaka 1998 Nigeria pia iliingia kwenye kombe la Dunia huku ikiwa na matumaini makubwa kwani kikosi kilikuwa na wachezaji karibu wote waliocheza kombe la dunia 1994 lakini bahati mbaya iliishia kucheza raundi ya pili katika hatua hiyo ya makundi, kama ilivyofanya kwenye michuano ya 1994.

    Hata hivyo katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002, Nigeria ilifanya vibaya kwani iliishia kwenye raundi ya kwanza na kutolewa kwenye michuano hiyo. Mwaka 2010 Nigeria pia ilifanya vibaya kule Afrika Kusini, kwani pia ilitolewa katika hatua ya makundi bila ya kuingia raundi ya pili. Ilipofika Juni 30 2010 rais wa Nchi hiyo Goodluck Jonathan, aliisimamisha nchi hiyo kushiriki kwenye michuano ya kimataifa kwa miaka miwili kutokana na kufanya vibaya, kitendo ambacho kiliingiza timu hiyo kwenye hatari ya kufungiwa na FIFA kwa sababu za kisiasa. Ingawa katika michuano iliyopita haikufanya vizuri Nigeria safari hii imepata nafasi nyingine ya kuonesha makeke yake kule nchini Brazil, tutegemee safari hii itajifunza kutokana na makosa ya nyuma, na kuweza kufika nafasi nzuri.

    Timu ya taifa ya Nigeria inaongozwa na kocha Stephen Keshi, ambaye amejipatia sifa kama kocha mwenye uwezo mkubwa, na kuchagua wachezaji nyota maarufu duniani jambo limeifanya timu hiyo ifanye vizuri kwenye michezo ya mwaka jana ya kombe la mataifa ya Afrika CAF, na tokea hapo imekuwa na matumaini kidogo, huku mchezaji wa Chelsea John Obi Mikel akiachana kabisa na mambo ya nyuma katika timu yake ya taifa na sasa kuwa mtu nayefanya vizuri zaidi. Kwa upande wa Vincent Enyeama naye pia veterani wa kutegemewa, huku Victor Moses, Ahmed Musa na Emmanuel Emenike wakiwa ni wachezaji imara kwenye upande wa ushambiliaji.

    Kocha wa timu ya Nigeria Stephen Keshi amepata mafanikio mbalimbali katika timu alizoziongoza katika mashindano ya FIFA, yakiwemo yale ya mwaka 1994 katika kombe la dunia lililofanyika Marekani ingawa haikufika robo fainali lakini ilifika kwenye raundi ya pili. Mwaka 1998 kwenye kombe la dunia la Ufaransa pia ilifika kwenye raundi ya timu 16. kwa upande wa michuano ya FIFA ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 iliyofanyika hapa China, na ile ya Japan mwaka 1993 pamoja na Korea Kusini mwaka 2007 walichukua ubingwa. Mafanikio hayo hayakuishia hapo bali katika michezo ya Olimpiki ya Atlanta timu yake ya soka ilipata ushindi, na katika michuano ya FIFA kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kule Saudi Arabia mwaka 1989 na Uholanzi mwaka 2005 ilichukua nafasi ya pili.

    Wachezaji wa kukumbukwa kwenye timu hii ni pamoja na Jay Okocha, Nwankwo Kanu, Rashidi Yekini

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako