• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchambuzi wa timu ya Ghana

    (GMT+08:00) 2014-05-21 15:23:11
    Wiki iliyopita katika kipindi hiki cha Jamvi uchambuzi wa timu za Afrika zitakazocheza kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil, tuliizungumzia timu ya taifa ya Nigeria "Super Eagle" jinsi ilivyoweza kufuzu michezo ya safari hii na jinsi ilivyofanya vibaya katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 kule Korea kusini na Japan na mwaka 2010 kule Afrika Kusini, hadi rais wa Nchi hiyo Goodluck Jonathan, aliisimamisha timu hiyo kushiriki kwenye michuano ya kimataifa kwa miaka miwili kutokana na kufanya vibaya, Pia tulisema kuwa ni timu ambayo haijavuka hatua ya makundi katika safari zake zote mbili ilizoshiriki michuano hii mikubwa na tulieleza mafanikio mbalimbali iliyopata katika michuano mbalimbali duniani. Sasa katika kipindi cha leo tutaizungumzia timu ya Ghana (nyota weusi) au "the Black Stars" na kuona jinsi ilivyofanya katika michuano iliyopita ya kombe la dunia lakini kabla ya kuendelea mbele tusikilize

    Sasa tunaendelea na uchambuzi wetu wa timu ya Ghana. Safari hii Ghana imeweza kuhimili vishindo vikubwa kabisa katika hatua ya makundi kwenye michuano ya kufuzu ya kombe la mataifa ya Afrika, kwani ilishinda mechi tano kati ya sita dhidi ya Zambia ambao ni mabingwa wa kombe hilo mwaka 2012, Lesotho na Sudan. Hata hivyo Ghana ilishuhudia kichapo cha 1-0 ilipocheza nchini Zambia na kupelekea kuzorotesha kampeni yao ya kumaliza michuano hiyo bila kufungwa Mechi hata moja. Kutokana na kufanya vizuri ilifikia hatua ya mtoano na baadae kuvaana na mabingwa wa mara 7 wa kombe la Afrika Mafarao wa Misri. Ushindi wa 6-1 walipocheza nyumbani kwao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya mafarao hao uliwawezesha kuingia kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mara ya tatu hata kabla ya kufungwa 2-1 huko Cairo katika mechi ya marudiano.

    The Black Stars wamefuzu mara tatu kwenye mashindano ya kombe la dunia ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006 ile ya Ujerumani, mwaka 2010 ya Afrika Kusini na safari hii nchini Brazil. Mwaka 2006 iliweza kuwapa kipigo Jamhuri ya Czech na Marekani kabla ya kutolewa na Brazil katika raund ya pili na kwa mwaka huo ilikuwa ni timu pekee ya Afrika iliyofika raundi ya pili. Mwaka 2010 pia ilikuwa ni nchi pekee ya Afrika kufika hatua ya mtoano na ilicheza vizuri kabisa ikilinganishwa na timu nyingine za Afrika kwa kuifunga Marekani na kufikia robo fainali. Hata hivyo Ghana ilipoteza wakati wa penalt dhidi ya Uruguay na kupelekea Asamoah Gyan kuondoa matumaini ya timu ya Afrika kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza, baada ya kukosa penalty.

    Ghana ilikuwa nchi pekee kufikia hatua nzuri kabisa ya raundi ya pili kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Ujerumani na ilikuwa nchi ya sita kutoka Afrika kufanikiwa kucheza zaidi ya hatua ya makundi kwenye michuano hiyo mikubwa. The Black Stars walikuwa na timu yenye wachezaji wadogo katika michuano ya mwaka 2006, ambapo kwa wastani wachezaji walikuwa na miaka miaka 23, na walipongezwa sana kwa uchezaji wao mzuri. Katika viwango vya FIFA, Ghana imewekwa ya 12 kati ya timu 32 zinazocheza mashindano ya kombe la dunia, na kwa michuano ya mwaka 2010 Ghana ilikuwa nafasi ya 7 katika viwango vya FIFA. Katika michuano ya mwaka huu Ghana ipo kwenye kundi G, pamoja na Ujerumani, Marekani na Ureno ambapo mchezo wake wa awali utapigwa tarehe 16 ya mwezi June dhidi ya Marekani kwenye uwanja wa Estadio das Dunas.

    Timu ya Ghana ina wachezaji mashuhuri kama ilivyo kwa timu nyingine nyingi za Afrika zinazoshiriki michuano hiyo kombe la dunia. Kuna wachezaji viungo kama vile Michael Essien na Sulley Muntari pamoja na wachezaji wengine nyota kama vile Andre Ayew, Kwadwo, Asamoah na Kevin-Prince Boateng. Mshambuliaji Asamoah atakuwa akianhgaliwa zaidi, ambapo na safari hii Ghana pia watataka kuthibitisha kuwa ni vinara kati ya timu za Afrika.

    Kwa upande wa kocha, kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kinaongozwa na Kwesi Appiah ambaye naye kama walivyo makocha wengi amepata mafanikio makubwa, yakiwemo mashindano kombe la dunia mwaka 2010 ambapo Ghana ilifika robo fainali. Michuano FIFA kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Italy mwaka 1991 na Equador mwaka 1995 ambapo walikuwa washindi. Mbali na hayo michuano ya FIFA kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kule nchini Misri mwaka 2009 pia walikuwa mabingwa na safari hii ameiwezesha timu kufuzu michuano hiyo.

    Wachezaji waliovuma sana wakati huo ni pamoja na Abedi Pele, Samuel Kuffour na Ibrahim Sunday.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako