• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Nigeria

    (GMT+08:00) 2014-05-22 15:45:48

    Timu ya Nigeria ambayo iliwahi kuwa na wachezaji maarufu kama Nwankwo Kanu na Augustine Okocha, ni moja ya timu zilizoonesha kuwa na nguvu barani Afrika katika miaka iliyopita. Iliwahi kuwa moja kati ya timu zilzofikia hatua ya timu 16 kwenye fainali za kombe la dunia kwa mara mbili. Mwaka 2010, timu ya Nigeria ilishindwa katika michuano ya makundi. Na katika miaka ya hivi karibuni, timu hiyo haikuonesha umahiri mkubwa barani Afrika. Mwaka huu itakuwa mara ya tano kwa timu hiyo kushiriki kwenye kombe la dunia, na itaendelea kupigania heshima yake.

    wanasoka maarufu wa timu ya Nigeria: Mikel John Obi

    Mwanasoka maarufu ya timu ya Nigeria ni kiungo John Obi Mikel wa timu ya Chelsea. Washambuliaji ni pamoja na Victor Moses wa timu ya Liverpool, Victor Nsofor Obinna wa timu ya Lokomotiv Moscow na Shola Ameobi wa timu ya Newcastle United. Kipa wa timu ya Lille OSC ambaye pia ni nahodha wa timu ya Nigeria Vincent Enyeama, alishiriki kwenye kombe la dunia la Korea Kusini na Japan mwaka 2002, pia amefanya vizuri katika michuano ya makundi ya kombe la dunia la Afrika Kusini mwaka 2010.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako