• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cameroon

    (GMT+08:00) 2014-05-22 15:50:31

    Watu bado hawajamsahau Roger Mila, ambaye ni mchezaji hodari kabisa katika historia ya timu ya Cameroon kwenye michuano ya Kombe la dunia. Timu ya soka ya Cameroon ya hivi sasa pia ina wachezaji wengi hodari akiwemo Samuel Eto'o. Timu ya Cameroon inasifiwa kuwa "Simba wa Afrika", imewahi kushiriki kwenye michuano ya Kombe la dunia mara sita, na ni timu iliyoshiriki kwenye fainali za michuano hiyo mara nyingi kuliko timu nyingine za Afrika, vilevile ni timu ya kwanza ya Afrika kufikia hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Kombe la dunia.

    Wachezaji

    Timu ya Cameroon ina wachezaji wengi hodari, Samuel Eto'o ni nahodha wa timu hiyo ambaye amewahi kucheza kwenye michuano ya Kombe la dunia ya mwaka 1998 nchini Ufaransa. Hivi sasa anachezea klabu ya Chelsea ya Uingereza. Mbali na Samuel Eto'o, timu ya Cameroon ina mchezaji wa kiungo Alexandre Song Billong anayechezea klabu ya Barcelona na mlinzi Stephane M'Bia wa klabu ya Sevilla ya Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako